1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mladic kushtakiwa rasmi Ijumaa ijayo

1 Juni 2011

Mkuu wa zamani wa jeshi la Serbia katika Bosnia, Ratko Mladic alitumia madaraka yake kufanya ukatili uliotenganisha taifa na kuteketeza jamii. Anapaswa kuwajibika kwa uhalifu huo amesema mwendesha mashtaka mkuu wa ICTY.

https://p.dw.com/p/RRKM
The aircraft believed to be carrying war crimes suspect Ratko Mladic is towed into a hanger having landed at Rotterdam Airport, Netherlands, after a flight from Belgrade, Serbia, Tuesday, May 31, 2011. War crimes suspect Ratko Mladic is on his way to The Hague, the Serbian justice minister said, just hours after judges rejected his appeal Tuesday to stop his extradition to a U.N. tribunal. (Foto:Bas Czerwinski/AP/dapd)
Ndege inayodhaniwa kumpeleka Ratko Mladic UholanziPicha: AP

Ratko Mladic atafikishwa mbele ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa mjini The Hague, Ijumaa ijayo. Hiyo ni hatua ya kwanza katika utaratibu wa kisheria dhidi ya Mladic aliekuwa mbioni kwa takriban miaka 16. Yeye anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya Bosnia kati ya mwaka 1992 na 1995.

Mashtaka hayo yamerekebishwa kuwa 11 badala ya 15 sawa na kiongozi wa zamani wa Serbia Radovan Karadzic aliefkishwa mahakamani kwa uhalifu huo huo. Mwendesha mashtaka wa ICTY, Serge Brammertz alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi habari alieleza kwanini Mladic anapaswa kufikishwa mahakamani:

"Yeye alikuwa mkuu wa jeshi mwenye mamlaka makubwa kabisa katika Bosnia wakati wa vita. Anashtakiwa uhalifu ulioshtua hisia za jamii ya kimataifa. Uhalifu wake unaashiria ukatili wa vita vya Bosnia na Herzegoniva."

Amesema, uhalifu wake umesababisha mtengano wa taifa na umevunja jamii. Miaka 16 ni muda mrefu kuongejea kuona haki ikitendeka. Sasa anapaswa kuwajibika kwa uhalifu huo mkubwa. Brammertz akaongezea:

" Tunajua kuwa jukumu muhimu liko mikononi mwetu. Nina hakika kuwa kesi hiyo itakuwa ya haki na itaheshimu heshimu haki zake. "

FILE In this June 28, 1996 file photo Bosnian Serb military commander General Ratko Mladic, center, smiles as he visits troops to mark both the fourth anniversary of the founding of his Bosnian Serb army and St. Vitus' Day, the anniversary of the Serb defeat by the Turks at Kosovo in 1389, near the village of Han Pijesak, some 40 miles east of Sarajevo. Belgrade media reports Thursday May 26, 2011 that a man suspected to be Europe's most wanted war crimes fugitive Ratko Mladic has been arrested in Serbia. Serbia state TV said a man who identified himself as Milorad Komadic when he was arrested Thursday is the wartime Bosnian Serb army commander. It gave no other details. (AP Photo)
Ratko Mladic alieongoza majeshi ya Serbia katika BosniaPicha: AP

Mladic alishtakiwa na mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa tangu miaka16 iliyopita. Mashtaka hayo yamehusika na mauaji ya wanaume na vijana wa Kiislamu 8,000 katika mji wa Srebrenica na kwa kuuzingira mji mkuu wa Bosnia Sarajevo kwa miezi 43 wakati wa vita vya Bosnia kati ya mwaka 1992 na 1995.

Mladic alikamatwa kijijini Lazarevo, kaskazini mashariki ya Serbia, Alkhamisi iliyopita na alipelekwa The Hague Uholanzi katika ndege maalum ya serikali ya Serbia jana jioni. Mshtakiwa huyo kwa mara ya kwanza atafikishwa mahakamani mbele ya majaji watatu kujibu mashtaka yanayomkabili.

Majaji hao ni Christoph Flügge wa Ujerumani, Alphons Orie kutoka Uholanzi na Bakone Moloto wa Afrika Kusini. Siku hiyo, Mladic atapaswa kujibu iwapo anakubaliana na mashtaka yanayomkabili. Iwapo atakanusha mashtaka hayo, basi atapewa muda siku 30 kufikiria upya . Kupitia mwanae wa kiume Darko Mladic, jenerali huyo wa zamani ameshasema kuwa yeye ahusiki kabisa na mauaji yaliyotokea Srebrenica.

Matayarisho ya kesi hiyo dhidi ya Mladic huenda yakachukua miezi kadhaa au hata mwaka mzima.

Mwandishi: Martin,Prema/rtre

Mhariri: Abdul-Rahman