1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wang Bin ahukumiwa maisha kwa kosa la rushwa

13 Septemba 2023

Mkuu wa zamani wa kampuni kubwa ya bima ya China,Wang Bin,amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na ufisadi.

https://p.dw.com/p/4WHJK
Prozess gegen Verleger Lai in Hongkong
Picha: Liau Chung-ren/ZUMA Press Wire/picture alliance

Shirika la habari la Xinhua limeripoti kwamba,Wang Bin aliyekuwa mwenyekiti na mkuu wa chama cha Kikomunisti katika kampuni ya bima ya China, alihukumiwa adhabu ya kifo ambayo itabadilishwa baada ya miaka miwili na kufungwa maisha kwa kosa la kuchukuwa hongo na kuficha akiba yake nje ya nchi. 

Shirika la habari la Xinhua limeripoti kwamba mahakama ya mkoa wa mashariki wa Shandong imemkuta Wang Bin na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake katika taasisi mbali mbali za fedha katika kipindi cha miongo kadhaa, akijipatia mamilioni ya dola kinyume cha sheria.

Tangu kuingia madarakani mwaka 2012 rais Xi Jinping China imeshuhudia kampeini kubwa dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wanaohusishwa na rushwa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW