Mkuu wa waasi wa Mai Mai aliyehusika na ubakaji akamatwa Kongo
6 Oktoba 2010Matangazo
Nchini Kongo kamanda wa kundi la waasi wa Mai Mai Cheka amekamatwa katika operesheni ya Umoja wa Mataifa na wanajeshi wa serikali iliyofanyika eneo la Mashariki mwa Nchi hiyo. Muasi huyo anatuhumiwa kuhusika na visa vya ubakaji wa kiasi ya zaidi ya wanawake 300 wakaazi wa eneo la Mashariki ya Kongo. Uhalifu huo ulitokea katika miezi ya Julai na Juni.
Mwandishi: John Kanyunyu
Mpitiaji:Thelma Mwadzaya