1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mkuu wa utumishi wa kiongozi wa kijeshi Mali auawa

20 Aprili 2023

Mkuu wa utumishi wa kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Mali ni miongoni mwa watu wanne waliouawa katika shambulizi la leo.

https://p.dw.com/p/4QMmR
Symbolbild Islamisten in Burkina Faso
Picha: ROMARIC OLLO HIEN/AFP/GettyImages

Oumar Traore, mkuu wa utumishi wa Kanali Assimi Goita, aliuawa katika shambulizi lililofanywa kaskazini mwa mji mkuu Bamako karibu na mpaka wa Mauritania, katika eneo linalofahamika kuwa na wanamgambo wa itikadi kali. Taarifa ya kutoka ofisi ya rais imesema mazishi yatafanywa leo katika mji ulio na kambi ya kijeshi wa Kati, karibu na mji mkuu Bamako. Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo. Mali imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kiusalama na kisiasa tangu uasi wa itikadi kali na wa makundi yanayotaka kujitenga ulipozuka kaskazini mwa nchi mnamo mwaka wa 2012. Tangu mwaka wa 2020 imekuwa chini ya utawala wa kijeshi unaoongozwa sasa na Kanali Assim Goita.