Mkuu wa UNDP Somalia auwawa
7 Julai 2008Matangazo
MOGADISHU
Watu wasiojulikana wamempiga risasi na kumuua mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Somalia Osman Ali Ahmed.Afisa huyo wa ngazi ya juu kabisa katika umoja wa mataifa mjini Mogadishu alipigwa risasi mara kadhaa kichwani na kifuani wakati akitoka msikitini na kufariki baadae hospitali.Mwanawe wa kiume pamoja na mtu mmoja walijeruhiwa katika kisa hicho.Mashirika ya misaada yamepunguza shughuli zao katika mji huo hatari kutokana na kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usalama.Umoja wa Mataifa mara kadhaa umetowa wito kwa serikali ya mpito ya Somalia na wanamgambo wa kiisalamu kuwaacha wafanyikazi hao wa misaada waendeshe shughuli zao bila matatizo.