1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa Tume ya Ulaya ataka kuongeza uzalishaji wa silaha

30 Agosti 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema umoja huo haujafanya vya kutosha kuimarisha uwezo wa kutengeneza silaha zake, wakati huu kukiwa na mivutano ya siasa kilimwengu.

https://p.dw.com/p/4k7MD
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: FREDERICK FLORIN/AFP

Von der Leyen amesema jukumu la kwanza la Ulaya ni kuilinda Ulaya. Ameongeza kuwa wakati Muungano wa Kijeshi wa NATO ukisalia kuwa kitovu cha nguvu jumuishi ya kiulinzi bado wanahitaji nguzo imara ya Ulaya.

Amesema hayo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa kimataifa wa usalama wa GLOBESEC, jijini Prague, Jamhuri ya Czech.  

Soma pia:Mawaziri wa EU wajadili mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine

Ameisistiza Ulaya kuwa macho, akisema itakuwa inajidanganya ikiwa itadhani kwamba imefanya vya kutosha kuhusiana na usalama, akionya nusu ya pilli ya muongo itakumbwa na kitisho zaidi.