1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa shirika UNHCR ataka ufadhili wa UNRWA urejeshwe tena

18 Februari 2024

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahuduma wakimbizi, UNHCR,Filippo Grandi ametaka malipo yarejeshwe kwa shirika lake tanzu la kuwahudumia kutoa msaada wa kwa Wapalestina, UNRWA

https://p.dw.com/p/4cXfl
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi Filippo Grandi
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa UNHCR, Filippo Grandi akizungumza na mwandishi wa habari wakati wa mahojiano yake na AFP mjini Kyiv Januari 26, 2023.Picha: Sergei Supinsky/AFP

Israel imewashutumu wafanyakazi kadhaa wa UNRWA kuhusika katika vitendo vya kigaidi vilivyofanywa na Hamas tarehe 7 Oktoba. Ripoti hiyo imesababisha nchi kadhaa za Magharibi kusitisha ufadhili kwa UNRWA, wakiwemo wafadhili wakuu, Marekani na Ujerumani. Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema hali ni mbaya sana kwa watu watu wa Gaza. Akizungumza waandishi wa habari kandoni mwa mkutano wa kimataifa wa usalama wa Munich amesema maamuzi ya haraka yamefanywa katika kuendelea au kuanza tena ufadhili, likiwa ni jambo bora kwa ustawi wa maisha ya mamilioni ya watu. Aliongeza kusema UNRWA inajukumu kubwa katika eneo hilo ambalo haliwezi kutokelezwa na yoyote. Shirika hilo lilianzishwa mwaka 1949 kwa lengo la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina, uendeshaji wa vituo vya elimu na matibabu.