1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Mkuu wa shirika la waandishi wasio na mipaka RSF afariki

9 Juni 2024

Mkuu wa shirika la kimataifa waandishi habari wasiokuwa na mipaka - RSF Christophe Deloire amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 53. Deloire aliugua ugonjwa wa saratani

https://p.dw.com/p/4gpiI
Mkuu wa RSF Christophe Deloire
Deloire amehudumu kama mkuu wa RSF tangu mwaka 2012 na kulifanya kuwa "bingwa wa kutetea waandishi habari.Picha: Jana Call me J/ABACA/picture alliance

Shirika hilo lenye makao makuu yake mjini Paris, Ufaransa limesema katika taarifa kuwa Deloire amekufa kutokana na ugonjwa wa saratani. Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa Deloire ambaye ni mwandishi wa zamani wa gazeti na ripota wa televisheni, amehudumu kama mkuu wa shirika hilo la RSF tangu mwaka 2012 na kulifanya kuwa "bingwa wa kutetea waandishi habari.”

Soma pia: RSF yamshutumu rais wa Mexico kwa kushindwa kuwalipa waandishi wa habari

Katika salamu zake za rambirambi kupitia mtandao wa kijamii wa X, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema fani ya uandishi ilikuwa moyoni mwa Deloire. Kiongozi huyo wa Ufaransa ameongeza kuwa Deloire alipigania bila kuchoka uhuru wa habari na mijadala ya kidemokrasia. Nayo kamati ya kulinda maslahi ya waandishi wa habari iliyo na makao makuu yake mjini New York, CPJ imeandika kwenye mtandao wa X kuwa, "imehuzunishwa mno" na kifo cha Deloire.