Mkuu wa jeshi Sudan kukutana na rais wa Misri leo
5 Novemba 2024Ziara hiyo ya jenerali al Burhani ni ya kwanza nchini Misri tangu nchi hiyo ilipokanusha kuhusika katika mgogoro unaoendelea Sudan.
Kwa mujibu wa msemaji wa al Sisi,Burhani alitarajiwa kukutana kwa mazungumzo na kiongozi huyo.
Taarifa ya jeshi la Sudan ilisema rais wa Misri alimualika al Burhani kushiriki kwenye mkutano wa 12 wa jukwaa linalojadili masuala ya makaazi duniani ulioandaliwa na shirika la mpango wa makaazi la Umoja wa Mataifa-UN-Habitat.
Soma pia:Abdel Fattah al-Burhan kukutana na Rais wa Misri mjini Cairo
Ziara ya hivi karibuni kabisa ya Burhani nchini Misri ilikuwa mwezi Februari wakati alipokutana na al Sisi na kujadiliana juu ya malengo ya serikali yake ya kutaka kumaliza vita na kuanzisha mchakato wa amani na uthabiti.
Ziara hii ya al Burhani imekuja wakati wanaharakati wa kutetea demokrasia wakiripoti leo Jumanne kwamba raia 10 wameuwawa katika jimbo la Al Jazira,kwenye shambulio linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wa RSF.