1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa IAEA kuizuru Moscow

6 Februari 2023

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, Rafael Grossi, ataitembelea Urusi wiki hii, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4N8i2
IAEA Direktor Rafael Grossi
Picha: Joe Klamar/AFP/Getty Images

Naibu Waziri wa Masuala ya Kigeni yaUrusi, Sergei Ryabkov, amesema ziara hiyo italenga kujadili kwa kina uundwaji wa eneo salama karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini Ukraine na kuongeza kwamba Moscow ilitaraji juu ya majadiliano hayo.

Kwa mara kadhaa, shirika hilo la Umoja wa Mataifa limekuwa likionesha wasiwasi juu ya mashambulizi katika mtambo huo mkubwa barani Ulaya, ambao umeshuhudia mkururo wa mashambulizi ya makombora kuzunguuka eneo hilo, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.