SiasaUkraine
Mkuu wa IAEA akitembelea kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia
29 Machi 2023Matangazo
Rafael Grossi ambaye hii ni mara yake ya pili kukizuru kinu hicho tangu kilipokamatwa na wanajeshi wa Urusi mwaka uliopita, anasema ziara hii inakwenda sambamba na juhudi za kupunguza uwezekano wa kutokea ajali.
Urusi na Ukraine zimekuwa zikishutumiana kukishambulia kwa mizinga kinu cha Zaporizhzhia, na mkuu huyu wa shirika la IAEA amekuwa akizitaka nchi hizo mbili kufikia makubaliano ya kukilinda kituo hicho cha kinyuklia ambacho ndicho kikubwa zaidi barani Ulaya. Wakaguzi wa IAEA wamewekwa katika kinu hicho tangu mwaka jana, kufuatia hofu juu ya uwezekano wa kutokea mkasa mkubwa.