1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Turk ataka ulimwengu ukabili ukandamizaji

11 Desemba 2023

Umoja wa Mataifa umewatolea mwito viongozi wa dunia kufufua mwamko uliochangia kufikia rasimu ya dunia ya kuunga mkono haki za binadamu miaka 75 iliyopita, ili kukabiliana na ukandamizaji uliozagaa hivi sasa ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4a0UG
Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.
Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk.Picha: Martal Trezzini/dpa/picture alliance

Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema makubaliano hayo yaliyopatikana baada ya vita vya pili vya dunia yalipatikana matumaini ili kumaliza kabisa mzunguuko wa umwagaji damu pamoja na kuweka ahadi ya kuzingatiwa haki.

Aliuambia mkutano wa maadhimisho ya miaka 75 ya mkataba huo kwamba,  makubaliano hayo yaliyopitishwa Paris nchini Ufaransa Desemba 10 mwaka 1948 yalitowa mwelekeo wa amani duniani.