1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa haki wa UN aonya dhidi ya operesheni kamili Rafah

12 Mei 2024

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk amesisitiza kuwa mashambulizi kamili ya mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza kamwe hayapaswi kufanyika.

https://p.dw.com/p/4flDX
Mkuu wa haki za binaadamu wa UN Volker Türk
Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi mkubwa wa kufanyika operesheni kamili ya ardhini ya jeshi la Israel mjini RafahPicha: Martal Trezzini/dpa/picture alliance

Katika taarifa, Turk amesema kuwa maagizo ya hivi karibuni ya kuhama maeneo ya mji huo wa Rafah, yanaathiri takriban watu milioni 1 akitilia mashaka wanakostahili kukimbilia usalama wakazi wa eneo hilo.

Turk pia amesema kuwa amesikitishwa sana na hali inayozidi kuzorota kwa kasi katika ukanda wa Gaza, na kuongeza kuwa maagizo hayo ya kuhama yamewaathiri watu ambao tayari wanakabiliwa na kiwewe.

Mkuu huyo wa haki za binadamu, amesema miji inayopaswa kuwapokea watu hao waliopoteza makazi kutoka Rafah, imeharibiwa kabisa huku akielezea wasiwasi kuhusu ripoti za mashambulizi ya kiholelea ya makombora kutoka Gaza.

Pia ametoa wito kwa Israel na makundi yenye silaha ya Palestina kukubaliana kusitisha mapigano, na mateka wote kuachiwa huru mara moja.