Mkuu wa Airbus aonya dhidi ya kuimarika sarafu ya euro
23 Novemba 2007Matangazo
Mkuu wa kampuni ya ndege ya Airbus barani Ulaya ameonya kwamba kupanda thamani kwa sarafu ya euro dhidi ya dola ya Marekani kunatishia kwa kiwango kikubwa sana maisha ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Thomas Enders amesema kwamba licha ya kuwepo kwa oda nyingi za ndege hiyo kampuni hiyo ya Airbus inategemea kupata hasara kubwa kutokana na athari za kubadilisha fedha.Mkuu huyo wa Airbus anasema kwamba hatua kali inabidi zichukuliwe na kwamba matumizi yote yale inabidi yaangaliwe upya.
Kampuni hiyo ya kutengeneza ndege tayari inafanya marekebisho yenye kukusudia kupunguza ajira 10,000 ifikapo mwaka 2010.