1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa UNCTAD wamalizika leo huko Accra,Ghana

25 Aprili 2008

Afrika sio kikapu cha kuombea misaada, lakini bara hilo linaungulika tu kutokana na athari za visa na mikasa ambayo haliwezi kuidhibiti.

https://p.dw.com/p/Doex
Mwenyekiti wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwenye mkutano wa UNCTAD huko GhanaPicha: AP

Hayo ni maneno ya mwanaharakati wa kutoka Togo, EKPLOM AFEKA, anayehudhuria mkutano wa 12 wa Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, unaofanyika mjini Accra, Ghana, tangu tarehe 20 mwezi huu hadi leo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, katika mkutano huo pia alivunjwa moyo na majaribio madogo sana yanayofanywa na jamii ya kimataifa kuengeza biashara na uwezekaji katika Afrika.

Bibi Hamida Maalim, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu huko Ghana, amehudhuria mkutano huo wa UNCTAD, akiwakilisha jumuiya isiokuwa ya kiserikali, na alimwambia Othman Miraji nini kile kilichoamuliwa katika mkutano huo wa Accra.