1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Umuhimu wa amazi utafanyika Zanzibar

15 Januari 2021

Kwa mara nyengine Zanzibar imekuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa utakaozungumzia umuhimu wa amani ikiwa ni mfululizo wa kushajiisha amani katika eneo hilo lenye migogoro ya kisiasa na kijamii.

https://p.dw.com/p/3nySi
Tanzania The Palace Museum, Stone Town
Picha: Peter Rchardson/robertharding/picture alliance

Mkutano huu wa siku mbili utakuwa na washikiri kutoka nchi nane za: Msumbiji, Malawi, DR Congo, Rwanda, Uganda, Burundi, Kenya, na Tanzania na mwenyeji Zanzibar katika baadhi ya maeneo ya nchi hizo wananchi hawana amani au wanaishi kwa wasiwasi kutokana na mivutano ya kisiasa au kijamii.

Kwa mujibu wa wandaaji na ratiba ya mkutano, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi amepangwa kufungua mkutano na pia makamu wake wawili Hemed Suleiman na Maalim Seif Sharif Hamad ambaye anatoka upinzani wamepangwa kuzungumza katika mkutano.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi Regina Heiss atakuwa miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo ambapo washikiri na watoa mada kutoka miongoni mwa wasomi wa dini, siasa, na jamii watachambuwa njia bora za kutunza Amani katika nchi zao.

Mkutano utazungumzia pia umuhimu wa Vijana kushajiisha na kuendeleza amani baada ya uchgauzi mkuu

Tansania Sansibar | Wahlen | Bevölkerung geht Wählen
Baadhi ya wakaazi wa visiwa vya Zanzibar Picha: Patrick Meinhardt/AFP/Getty Images

Miongoni mwa mada zitakazotolewa ni "Haja ya Vijana kushajiisha na kuendeleza amani baada ya uchgauzi mkuu' mada itakayotolewa na mwanasheria-wakili katika Mahakama kuu ya Kenya, Sheikh Ibrahim Lithome ambaye pia ni mkurugenzi wa masomo ya mikakati ya amani katika pembe ya Afrika.

Mada nyengine ni Uzoefu kutoka Rwanda baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994 itakayowasilishwa na balozi Saleh Habimana, kutumia ujasiri amali kama njia ya kuendeleza amani, na nafasi ya vyombo vya Habari katika kuendeleza amani nchini itakayowasilishwa na Dk Mustafa Ali kutoka Nairobi Kenya.

Migogoro mingi katika nchi za Afrika inatokana na chaguzi ambapo mwishoni mwa mwaka Tanzania imemaliza uchaguzi wake huku Uganda ikiwa umefanyika wiki hii na Kenya wanatarajia kufanyika uchaguzi mkuu mwakani.