Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa wakamilishwa leo
14 Desemba 2007Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa ukiwa unafikia mwisho wake leo,waziri wa mazingira wa Ujerumani anasema anataraji kuwa Ulaya itaweza kuondoa kizungumkuti na Marekani.Sigmar Gabriel amewambia maripota katika mkutano huo kuwa pande zote zinajaribu kutafuta wapi pa kukubaliana kuhusu upunguzaji wa utoaji wa gesi zinazochafua mazingira. Mwenyeji Indonesia, imependekeza katika hati ya mwisho, kifutwe kifungu kinazozitaka nchi zenye viwanda kupunguza kwa asili mia 40 utoaji wa gesi ifikapo mwaka wa 2020. katika kipindi cha wiki mbili cha mkutano huo,Ulaya na Marekani zimevutana kuhusu ratiba ya mwaka wa 2020.Marekani inapinga ratiba hiyo.
Mazungumzo ya Bali yana nia ya kuweka mwongozo wa utakao saidia mjadala wa miaka miwili wa kupata mkataba mpya wa halia ya hewa utakaochukua ule wa Kyoto unaomalizika mwaka 2012.