Mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO
14 Juni 2007Usoni katika ajenda yao ni hali iliozidi kuchafuka nchini Afghanistan.Katika mkesha wa mkutano huu, jamadari-mkuu wa NATO, mjerumani Egon Rams alitoa maneno makali juu ya hali huko Afghanistan.
Mezani mwa mawaziri wa ulinzi wa NATO hali nchini Afghanistan ni tofauti kabisa na ilivyo miongoni mwa maamirijeshi wake.Tangu Januari mwaka huu, jamadari Egon Ramms, mjerumani ndie anaeongoza kituo kikuu cha NATO huko Brunssum,Holland,si mbali na mpaka na Ujerumani.Ameshika dhamana muhimu kabisa katika shirika la ulinzi la magharibi –NATO.Kwani ni chini ya uongozi wakwe tangu 2003 mipango yote ya kutumika kwa vikosi vya NATO nchini Afghanistan (ISAF) inakopitia.
Ni jamadari Ramms anaewasiliana na makao makuu ya NATO mjini Kabul,Afghanistan.
Hali ya usalama imezidi kuharibika hasa kaskazini ambako ndiko vikosi vya Ujerumani vya bundeswher vinatumika.
Jamadari Ramms asema:
“Naamini kutokana na matokeo jumla ya vita vya vikosi vya ISAF huko kusini mwa Afghanistan ,sura ya vita yaweza kuwa imebadilika.Yatupasa pia kuchukulia kuwa Watalibani na waalqaeda wanajiandaa barabara na kujitanua.Na ikiwa umesikiliza mjadala kwetu Ujerumani,yawezekana watalibani hao wakaitumia hali hiyo kufanya hata mashambulio zaidi.”
Alionya Jamadari Ramms.
Kuwaua askari zaidi wa Bundeswehr ni kuutilia shaka-shaka mkatano wa NATO huko Afghanistan.Jamadari Ramms anabainisha dhahiri shahiri kuwa, vikosi vya Ujerumani huko Afghanistan vinapaswa sasa kujiwinda zaidi kujikinga na hujuma.
2.O-Ton Ramms
“Wakanada wanatumia vifaru katika opreshini zao huko Afghanistan.Waholland wamekwenda na aina ya magari ya vifaru 2ooo ili kujikinga na hujuma za moja kwa moja za maadui.Isitoshe, yafaa mtu kujiandaa kuwa kinga kama hiyo inahitajika pia kwa vikosi vya Ujerumani.”
Nchi zanachama wa NATO zimechangia kiasi cha wanajeshi 40.000 wanaopigana nchini Afghanistan na sehemu kubwa yao wako chini ya paa la vikosi vya ISAF vyenye jukumu hasa la kuijenga upya Afghanistan.
Sambamba na jukumu hilo, askari 8000 wengiwao wamarekani, wanapigana na magaidi nchini Afghanistan katika opertesheni “Enduring freedom.” (OEF).ISAF na OEF kila kukicha zinafanya kazi pamoja.
Kwahivyo, madai ya majamadari na maamirijeshi kwa wanasiasa hayamaliziki na hali ni vivyo hivyo katika kikao hiki cha leo na kesho huko Brussels katika mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO.