Mkutano wa masuala ya ustawi wa jamii ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia
17 Aprili 2007Matangazo
Kikao hicho kinahusisha wawakilishi wa serikali, vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kujadilia masuala mbalimbali ya kuimarisha ajira vile vile kupambana na changamoto zinazotokana na utandawazi.
Mwandishi wetu wa Addis Abeba Anaclet Rwegayura alizungumza na Dr.Aggrey Mulimba mkurugenzi mtendaji wa chama cha waajiri nchini Tanzania anayehudhuria mkutano huo wa siku tatu.