1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Nairobi

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsF

Nairobi:

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ameonya mabadiliko ya hali ya hewa ni kitisho kwa amani na usalama ulimwenguni.Akihutubia mkutano wa mjini Nairobi kuhusu hali ya hewa,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ameitaka jumuia ya kimataifa ilishughulikie suala la mabadiliko ya hali ya hewa sawa na inavyoshughulikia juhudi za kuepusha vita,mapambano dhidi ya silaha za maangamizi na umasikini.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan amesema:

„Sote tunataka pawepo dunia inayowavutia viumbe wote na kuhakikisha uwiano kati yao na mazingira ya kimaumbile ambayo tunayahitaji ili kuweza kuishi.“

Mkutano wa hali ya hewa umeingia katika awamu muhimu wiki hii.Mawaziri wa mazingira kutoka nchi kadhaa wanapanga kujadiliana juu ya rasimu ya pili ya Kyoto.Waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani Sigmar Gabriel akihutubia mjini Nairobi amesema nchi zinazoinukia zisilazimishwe tuu kupunguza moshi wa viwandani bila ya kubuniwa njia zitakazoziruhusu nchi hizo kufanya hivyo bila ya kuathiri ukuaji wa kiuchumi.