1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa EU

19 Juni 2008

Umoja wa Ulaya umeanza mkutano wake wa kilele mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/EMpB
Angela Merkel (kulia)Picha: AP

Viongozi wa nchi zanachama wa Umoja wa ulaya, wanakutana leo mjini Brussels,Ubelgiji wakivinjari kuonesha kuwa Ulaya inaweza kutatua matatizo yake magumu -kama vile kukataliwa na Jamhuri ya Ireland mkataba wa Lisbon na kupanda mno bei ya mafuta.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, nae amesema leo kuwa Umoja wa Ulaya, unauhitaji mkataba wa Lisbon na hivyo, lazima uidhinishwe na wanachama wote tenakwa kauli moja.

►◄Viongozi hao 27 wa dola na serikali wa Umoja wa ulaya,walitiwa jeki jana usiku pale Bunge la Uingereza lilipo uidhinisha mkataba wa Umoja huo uliotiwa munda majuzi na kukataliwa na wapigakura wa Jamhuri ya Ireland.

Mkataba huo unalenga kuzileta taasisi zinazoyumba yumba za Umoja huo katika muundo wa kisasa.

Baada ya mjadala motomoto Baraza la House of Lords lilkauidhinisha mkataba huo.Uingereza mojawapo ya wanachama wa kaidi na mwenye shaka-shaka na Umoja huo,imekuwa kwahivyo dola la kwanza kuidhinisha mkataba tangu pale wapigakura kuukataa kupitia kura ya maoni.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani amesema leo kuwa umoja wa Ulaya, unauhitaji Mkataba huu na kwahivyo, lazima uidhinishwe tena kwa sauti moja ya wanachama wote 27.

Kanzela Merkel alisema hayo kabla mkutano huu wa leo na kesho wa kilele mjini Brussels kufuatia kupigwa teke na wapigakura wa Ireland hatua ambayo ilizusha msukosuko wa taasisi zake. Angela Merkel aliliambia Bunge la Ujerumani kuwa Ujerumani, haikubaliani asilani na Ulaya inayoendelea kwa kasi tofauti.

Kabla mkutano wa kilele wa hii leo, spika wa Bunge la Ulaya,mjerumani Pöttering alisema:

"Sitarajii kumalizwa matatizo yote yaliozuka,bali nataraji leo kuanza kuyatatua na kuwa Bunge la Ulaya, nitalibainishia wazi leo linavyopaswa kutoa mchango wake."

Spika huyo wa bunge la Ulaya akasisitiza zaidi:

"Tunasema pia kuwa tunataka mkataba huu wa mageuuzi unalazimika kuidhinishwa ili mambo yasonge mbele."

Ili kubainisha kuwa mkataba huu haukuzikwa na kura ya kuukataa ya waireland,viongozi wa Umoja wa Ulaya wametia nia kuhakikisha nchi 8 zanachama ambazo bado hazijauuidhinisha mkataba huo, zifanye hivyo kupitia kura ya Bungeni.

Mawaziri wa nje wa UU wakikutana mjini Luxembourg jumatatu, waliahidi kuipa Jamhuri ya Ireland muda na wasaa kusaka kujitoa kutoka msukosuko iliojiingiza na hakuna anaetazamia kuwa njia rahisi.

Hatahivyo, viongozi wa UU wana azma ya kutunga mpango hadi Oktoba-kwa muujibu wasemavyo wajumbe wao wa kibalozi-kuepusha Umoja wao kujitosa katika mzozo kama ule uliofuatia rasimu ya katiba na kupeelekea mkataba wa Lisbon kutungwa kuchukua nafasi yake.Mara hii wanachama 27 wa UU wana hamu kuonesha kwamba wangali wakikodolea macho shabaha muhimu ya wakati huu kwa kuongoza wa Umoja wa Ulaya na sio kujadiliana vipi kuongoza.

Kwahivyo, mbali na mada ya mkataba , mzozo wa bei za juu za nishati na hasa mafuta ya petroli pamoja na chakula ni maswali yaliopo usoni mwa ajenda ya kikao cha leo mjini Brussels.