Mkutano kati ya Ujerumani na Afrika wamalizika Afrika Kusini
9 Desemba 2022Uwezekano wa Ujerumani wa kuwekeza barani Afrika umepigiwa debe kwenye mkutano huo.
Mkutano huo ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, huwaleta pamoja viongozi wa serikali na wafanyabiashara wa Afrika na Ujerumani. Kwa Ujerumani, mkutano huo ni tukio kubwa kabisa la kibiashara barani Afrika.
Nusu ya vitega uchumi kutoka Ujerumani vinaelekezwa nchini Afrika Kusini ambako kampuni zaidi ya 400 za Ujerumani zinatoa ajira kwa watu wapatao 65,000.
Waziri wa uchumi wa Ujerumani Robert Habeck alipoufungua mkutano huo alisema kampuni za Ujerumani ziliwekeza dola bilioni 1.6 kwenye nchi za Afrika.
Hata hivyo ameeleza kuwa kiwango hicho bado hakijatosheleza. Habeck ametoa wito wa mtazamo mpya katika uhusiano kati ya Ujerumani, barala Ulaya na lile la Afrika.