Mkutano wa kibiashara wa wanawake mjini Berlin
18 Juni 2007Zaidi ya wanawake Elfu moja,mkiwemo mawaziri 50 kutoka nchi 91, walihudhuria kikao hicho cha Biashara cha 17 ambapo Rais wa kikao hicho Bi Irene Natividad raia wa US mwenye asili ya kifilipino aliwambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo kua, wanawake ndio viongozi wa leo wanaosaidia kubadilisha mfumo wa kiuchumi katika karne ya 21.Bi Natividad aliongeza kusema wanawake waleo wameendelea kiilimu na kuwakilishwa katika kazi nyingi duniani kuliko wanaume, hii ikiwa asili mia 40 hadi 50. Hata hivo Bi Natividad alikubali kua wanaume bado wanalipwa uzuri zaidi, ukilinganisha na wanawake lakini hilo halitowazuwia kuleta maendeleo zaidi.
Katika mkutano huu wa kibiashara,nchi za bara la Asia, Vietnam na Uchina, ndizo zilizowakilishwa na wajumbe wengi. Akiongoza ujumbe wa watu 52, Makam Rais wa Vietnam, Truong My Hao alisema mkutano huu ulikua muhimu sana kwa Vietnam kupata soko katika utandawazi wa kibiashara, na sasa itakabiliwa na changamoto za kibiashara ilivokua ndio kwanza Vietnam, imekubaliwa kuwa mwanachama wa shirika la Biashara Duniani (WTO)
Makam Rais wa Vietnam alisema wakati wa vita nchini Vietnam, wanawake walishiriki kwenye harakati za kupigania uhuru wa nchi yao, na wakati huu wa Amani, wanawake wamechangia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
Hata hivo tatizo la ilimu kwa wanawake nchini Vietnam ni finyo sana, ukilinganisha na wanaume, na pia bado wanaume ndio wanaopokea mishahara minono kwa saabu ndio wenye ilimu bora.
Mkutano huu ulihudhuriwa pia na Bi Sung- Joo Kim mfanya biashara maarufu kutokea Korea Kusini ambae alisema yeye aliamua kuanzisha biashara yake mwenyewe bada ya babaake kufariki dunia na kiwango kikubwa cha utajiri wake walipewa ndugu zake wa kiume kwa sababu tabia ya nchi ya Korea Kusini kila kitu hudhibitiwa na wanaume.
Sung-Joo Kim anasema kwa miaka miwili iliopita biashara yake ya kuuza vifa vya ngozi kama Begi za kike n.k ilifikia dola Millioni Mia Moja ikiwa na wafanya kazi Mia 5 katika maduka zaidi ya 100 duniani, duka la Harrods la mjini London nchini Uingereza likiwa moja wapo linalouza bidhaa zake.