MKutano wa jumuia ya NATO mjini Sofia
28 Aprili 2006Mataifa 26 yanachama wa jumuia ya kujihami ya magharibi NATO hayajakubaliana bado juu ya uwezekano wa kuendelezwa ushirikiano pamoja na mataifa ya Asia na Pacific .Katibu mkuu wa NATO,Jaap de Hoop Scheffer amesema baada ya siku ya kwanza ya mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nchi za nje mjini Sofia,mapendekezo tofauti yametolewa kuhusu ushirikiano wa siku za mbele pamoja na mataifa kwa mfano Australia,New-Zealand,Japan na Korea ya Kusini.Nchi hizo tayari zinashiriki katika shughuli za NATO nchini Afghanistan.Mbali na hayo mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa NATO wameshauriana pia juu ya ishara zinazobidi kutolewa na viongozi,wakati wa mkutano wao,msimu wa mapukutiko ujao,kwa zile nchi zinazoomba uanachama,yaani Albania,Kroatia,Macedonia,Georgia na Ukraine.