Mkutano wa Jukwaa la vyombo vya habari DW waanza Bonn
11 Juni 2018Washiriki 2000 wa kimataifa watajadili , vipi vyombo vya habari vinaweza kubadilisha hali hiyo na kuonesha kwa vitendo , jinsi wanavyoweza kufanya kupambana na hali hiyo ya kutokuwa na usawa.
Wakati viongozi wa kisiasa na kiuchumi, viongozi wa vyombo vya habari, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wataalamu wakifanyia kazi kalenda ya shughuli zao katika mwezi wa Juni , basi hutenga siku tatu , kwa kuwa shirika la utangazaji la Deutsche Welle linawakutanisha pamoja katika mkutano wa Jukwaa la vyombo vya habari, GMF. Mwaka huu kuanzia tarehe 11 hadi 13 Juni jukwaa hilo litajishughulisha na mada ya harakati za dunia, hali ya kutokuwa na usawa duniani.
Jukwaa la vyombo vya habari duniani, Global Media Forum, limekuwa sasa mkutano mkubwa wa kimataifa wa vyombo vya habari unaofanyika nchini Ujerumani kila mwaka. Wanatarajiwa wageni 2000 kutoka karibu nchi 120. Mkurugenzi wa DW Peter Limbourg anauchukulia mkutano huu wa Jukwaa la vyombo vya habari kuwa ni jukwaa la kipekee la kubadilishana mawazo baina ya waandishi habari kutoka nchi mbali mbali, pamoja na viongozi wa vyombo vya habari ambao ni washirika wetu duniani kote pamoja na watu ambao wanapambana kuwa na uhuru wa vyombo vya habari.
DW yaenea kila mahali
Na msimamo wa mkurugenzi Limbourg ni wazi , kwamba Jukwaa la vyombo vya habari linaonesha kila mwaka , vipi Deutsche Welle imeweza kuenea kila mahali. Tunaweza kujifunza mengi kupitia mijadala na kubadilishana mawazo.
Taarifa nyingi hususan kutoka Pakistan na Bangladesh pamoja na mataifa ya Afrika, anaripoti Verica Spasoviska , mwaka huu zinahusika katika kile kinachojadiliwa katika mada za mkutano huu.
Karibu waandishi habari 100 kutoka katika mataifa yaliyoendelea na yale yanayoinukia kiuchumi wanashiriki katika mkutano huo, kwa msaada mkubwa wa kufanyakazi kwa pamoja na wizara ya mambo ya kigeni, anasisitiza kiongozi wa shughuli za mkutano huo wa Global Media Forum, Guido Schmitz. Schmitz anaelezea kuhusu ushirikiano wa jukwaa hilo la vyombo vya habari GMF na jimbo la North Rhine Westfalia kuwa ni muhimu kwa mafanikio ya mkutano huo.
Mada hii ya kutokuwa na usawa duniani itakuwa na matukio karibu 60 katika mkutano huu , ambapo katika kiwango cha wanasiasa kwa mfano atazungumza kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na masuala ya digitali Mariya Gabriel. Ama pia kiongozi wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai, ambaye hapo kabla katika mahojiano na DW aliwahi kutoa matamshi ya kutatanisha. Ambapo alisema Karzai alizitupia lawama Pakistan na Marekani kwa matatizo yanayoikumba nchi yake. Pia anatarajiwa kuzungumza mwandishi habari Yusuf Omar , ambaye ni mwanzilishi wa ripoti kupitia simu ya mkononi , na ataeleza vipi simu ya mkononi inaweza kupambana na hali ya kutokuwa na usawa.
Mwandishi: Matthias Hein / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman