1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Hali ya Hewa wa UM wamalizika:

13 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFsa

Milan:Mwishoni mwa Mkutano wa Hali ya Hewa wa UM nchini Uitalia, wana mazingira na wanasiasa wamezidi kuishinikiza Urusi itie saini Mkataba wa Kyoto. Kutiwa saini mkataba huo kutaipatia manufaa Urusi ambayo itapatiwa mikataba wa kibiashara na vitega uchumi vya kimataifa katika ufundi wa mazingira, alisisitiza Waziri wa Mambo ya Mazingira wa Ujerumani Jürgen Trittin mjini Milan. Pamoja na hayo, kufuatana na kuongezeka kwa athari za kupashika moto dunia lazima zichukuliwe hatua za haraka za kutafuta kinga. Kabla ya hapo UU ziliyaita mataifa yote ambayo bado hayakusaini Mkataba wa Kyoto kufanya hivyo. Lakini kama vile Marekani nayo Urusi inaendelea kupinga kuusaini Mkataba huo.