1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G8 mjini Berlin

Oummilkheir10 Septemba 2007

Moshi wa viwandani upunguzwe kwa asili mia 30 hadi mwaka 2020

https://p.dw.com/p/CH8L
Moshi wa viwandani waathiri mazingira
Moshi wa viwandani waathiri mazingiraPicha: AP

Mawaziri wa uchumi na wa mazingira kutoka nchi 20 zinazotumia nishati kwa wingi kabisa ulimwenguni wanakutana kuanzia leo mjini Berlin.Lengo la mkutano huo wa siku mbili ni kuyapa msukumo mazungumzo ya umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.Tangu mwaka 2005,mkutano wa kilele wa G8 ulipoitishwa huko Gleneagles Scottland,viongozi walikubaliana kuhimiza mijadala ya kisiasa kuhusu hali ya hewa ulimwenguni.

Wawaakilishi wa kutoka mataifa manane tajiri kwa viwanda pamoja na mawaziri wa kutoka China,India,Afrika kusini,Brazil,Mexico,Australia,Indonesia,Nigeria,Poland,Hispania na Korea ya kusini wanashiriki katika duru hii ya tatu ya “Mjadala wa Gleneagles” mjini Berlin.Wawakilishi wa benki kadhaa za maendeleo,taasisi ya kimataifa ya nishati na bodi ya Umoja wa mataifa inayosimamia masuala ya hali ya hewa nao pia wamealikwa kuhudhuria mkutano huo unaosimamiwa na waziri wa mazingira wa serikali kuu ya ujerumani Sigmar Gabriel na waziri wa fedha Michael Glos.

Kuna kitu kimoja ambacho waziri wa mazingira wa serikali kuu ya Ujerumani hakitaki nacho ni kuona kwamba ziara ya mawaziri wa nishati na mazingira wa kutoka kila pembe ya dunia hadi Ujerumani,haileti tija yoyote nyengine isipokua kua gharama za bure na moshi.Lazma watu wasonge mbele katika masuala kwa mfano ya kuyajumuisha mataifa yanayoinukia na yanayoendelea kiuchumi katika juhudi za za kupunguza moshi unaotoka viwandani:

“Mjadala wa Gleneagles” ulianza mwaka 2005 katika mji wenye jina hilo hilo huko Scottland.Nchi 20 zenye kutumia nishati kwa wingi kabisa ulimwenguni zinashiriki ,zikiwemo pia benki za maendeleo,taasisi ya nishati ya kimataifa,bodi ya umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya hali ya hewa na wawakilishi wa kiuchumi pamoja na mashirika yasiyo milikiwa na serikali.

Katika mkutano wa kilele wa G8 mjini Heligendamm ,karibu na Berlin,Marekani-dola linalotoa kwa wingi kabisa ulimwenguni moshi wa Carbon Dioxide,ilisema itakua tayari kujiunga na makubaliano ya kuhifadhi hali ya hewa chini ya usimamizi wa Umoja wa mataifa.Hivi sasa kipa umbele ni kuzitanabahisha nchi kama vile China na India zijiunge pia na makubaliano hayo-anasema waziri wa mazingira Sigmar Gabriel:

“Kipa umbele kwa sasa ni msimamo rasmi wa nchi zinazoinukia na zile zinazoendelea:hatujadiliani,tunazungumza tuu kuhusu majukumu ziada ya mataifa tajiri kiviwanda na kuendeleza midahalo chini ya misingi ya makubaliano ya kuhifadhi hali ya hewa.”

Muakilishi maalum wa Umoja wa mataifa anaeshughulikia masuala ya hali ya hewa,Gro Harlem Brundland,anahisi ni jukumu la mataifa tajiri kiviwanda kutoa pendekezo la maana kwa nchi zinazoinukia.Kiongozi huyo wa zamani wa serikali ya Norway ,ingawa anasifu juhudi za G8 na umoja wa ulaya za kuhifadhi hali ya hewa,hata hivyo anahisi hazitoshi kufikia ufumbuzi jumla ikiwa mataifa mengine hayatajumuishwa.

Katika mkutano huu wa Berlin,bibi Brundtland na viongozi wengine wa zamani wa taifa na serikali wanapanga kutoa mapendekezo yatakayoijongeza misimamo ya pande zote zinazohusika.Katika Ripoti yao ya kurasa 12,wanapendekeza moshi wa viwandani upunguzwe kwa asili mia 30 hadi ifikapo mwaka 2020-ikilinganishwa na mwaka 1990.

Pia pendekezo la kansela Angela Merkel kuhusu moshi wa viwandani na idadi yaakaazi wa nchi husika litajadiliwa katika mkutano huu wa siku mbili mjini Berlin..