1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G7 wamalizika Tokio

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4yc

Tokyo:

Mawaziri wa fedha na wakuu wa benki wa mataifa sabaa tajiri kiviwanda wakimaliza mkutano wao mjini Tokyo wamekumbusha changamoto na mitihani inayoukabili uchumi wa dunia.Ukuaji wa kiuchumi huenda ukazorota kwa muda-wameonya mawaziri hao katika taarifa yao ya pamoja.Mawaziri wa fedha na wakuu wa benki wameondowa hata hivyo uwezekano wa kuporomoka uchumi wa Marekani mnamo mwaka huu wa 2008.Kutokana na mzozo unaozikaba benki,mawaziri wa fedha wa mataifa tajiri kiviwanda wameyatolea mwito mashirika ya fedha yasifiche ukweli hasara inapopatikana na yafanye juhudi za kuimarisha rasli mali zao.Taarifa hiyo imesema mataifa tajiri kiviwanda yataendelea kuchunguza kwa makini hali namna ilivyo na kuchukua hatua zinazohitajika kuhifadhi ukuaji na utulivu wa kiuchumi.