1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa G7 kujadili uchumi unaozorota

9 Septemba 2011

Mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa mataifa saba tajiri duniani G7 wanakutana Ufaransa, chini ya shinikizo la kuchukua hatua za kuufufua uchumi unaozorota na kuyatuliza masoko ya fedha yaliyoingiwa wasiwasi.

https://p.dw.com/p/Rkj5
epa02639510 (FILE) A file photo dated 15 September 2010 of French Budget Minister Francois Baroin leaving the Elysee palace after the weekly cabinet meeting in Paris. Acting as government spokesperson, Baroin has told RTL radio on 18 March 2011 that France's participation in a military operation against the Libyan regime of Muammar Gaddafi after the resolution of the UN Security Council to be in 'hours'. 'The attacks will occur quickly,' advanced Baroin, in an interview with radio station RTL. He stressed that 'the French, of course, will be consistent' with which it has been their position and 'participate' in the operation. While declining to give details on when, how and of the nature of military objectives singled out for the operation, Baroin said that this is 'an intervention, and not an occupation, but a military action to protect the Libyan people.EPA/IAN LANGSDON +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa Fedha wa Ufaransa, Francois BaroinPicha: picture-alliance/dpa

Ufaransa, iliyo mwenyeji wa mkutano huo wa G7, imetoa mwito kuchukua hatua zilizoratibiwa na mataifa hayo tajiri, baada ya wasiwasi kuzuka kwa sababu ya mzozo wa madeni barani Ulaya na kusababisha thamani ya hisa kuporomoka vibaya katika masoko ya fedha hivi karibuni. Lakini matatizo tofauti ya kiuchumi yanayokabiliwa na Marekani, Uingereza na nchi za kanda inayotumia sarafu ya Euro, hutatanisha kazi hiyo. Hakuna ufumbuzi mmoja kwa matatizo yanayotofautiana.

Taarifa kutoka mjini Brussels Ubeligiji inasema, mkutano wa G7 huenda ukakubaliana sera ya kuendelea kuweka kiwango kidogo cha riba, kupunguza nakisi na madeni ya serikali, kule kunakowezekana na kufanya mageuzi katika mfumo wa uchumi. Waziri wa Fedha wa Ufaransa, Francois Baroin amesema, kila nchi katika kundi hilo la G7 ichukue hatua kuambatana na hali yake ya kiuchumi. Hapo awali, Waziri wa Fedha wa Marekani, Timothy Geithner alisisitiza kuwa ni lazima kuchukua hatua za kusaidia ukuaji wa kiuchumi.

United States Secretary of the Treasury Timothy Geithner speaks during a session at the World Economic Forum in Davos, Switzerland on Friday, Jan. 28, 2011. In a nod to the post-crisis atmosphere, the World Economic Forum shifts its attention on Friday to austerity measures and priorities for improving the economy. (Foto:Michel Euler/AP/dapd)
Waziri wa Fedha wa Marekani, Timothy GeithnerPicha: dapd

Kwa mujibu wa tathmini ya shirika la ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo OECD, ukuaji wa kiuchumi katika nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda, utapungua katika robo ya mwisho ya mwaka huu, ukilinganishwa na ukuaji wa miezi mitatu iliyopita. OECD imetoa mwito kwa viongozi wa G7 na magavana wa benki kuu, kuchukua hatua za kuchangamsha uchumi unaozorota .Benki Kuu zimehimizwa kuendelea na kiwango cha chini cha riba na kuzingatia hatua zingine za kusaidia ukuaji wa kiuchumi.

Japan inatazamiwa kuujadili mzozo wa madeni unaoakabiliwa na nchi za kanda inayotumia sarafu ya Euro barani Ulaya, wakati nchi za Asia zikiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu mzozo huo wa madeni katika nchi za magharibi pamoja na ukuaji wa kiuchumi unaozorota. Japan huenda ikaeleza wasiwasi wake kuhusu uimara wa sarafu yake Yen na ikajiamulia kuchukua hatua ya upande mmoja. Mkutano wa G7 nchini Ufaransa, umepewa umuhimu maalum kwa sababu ya hofu kuwa uchumi hivi sasa huenda unapitia kipindi kigumu kabisa, tangu ulipotokea mzozo wa fedha mwaka 2008 kote duniani.

Mwandishi: Martin,Prema/rtre

Mhariri:Mwadzaya, Thelma