Mkutano wa CDU waanza.
3 Desemba 2007Matangazo
Hannover.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefungua rasmi mkutano wa siku mbili wa kila mwaka wa chama cha Christian Democratic Union mjini Hannover. Katika mkutano huo , CDU inapanga kuimarisha nafasi yake na kutaka kujiweka mbali na mshirika wake katika serikali ya muungano chama cha Social Democratic. Chama cha CDU kimesema kitaweka umuhimu wa kujiweka katika nafasi ya mrengo wa kati katika siasa za Ujerumani katika mkutano huo wenye kauli mbiu inayosema chama cha mrengo wa kati. Suala muhimu ambalo inalikataa ni kiwango cha chini cha mshahara kama linavyopendekezwa na chama cha SPD mshirika wake katika serikali ya mseto. Ujerumani inatarajiwa kufanya uchaguzi wake mkuu mwaka 2009.