Wakuu wa nchi za Kiafrika wanakutana kwa siku ya pili nchini Mauritania, katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU), ambao miongoni mwa mada nyingine, unajadili mkakati wa kurejesha raslimali za Afrika zinazoporwa na kupelekwa nje, pamoja na vita dhidi ya makundi ya itikadi kali.