1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kujadili mustakabali wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu

18 Februari 2010

Nchi wanachama 47 wa Baraza la Ulaya wamekusanyika Interlaken nchini Uswisi kwa mkutano wa siku mbili unaonza hii leo kujadili mustakabali wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu iliyo na makao yake mjini Strasbourg.

https://p.dw.com/p/M4dB
Nchi wanachama 47 wa Baraza la Ulaya wamekusanyika Interlaken nchini Uswisi kwa mkutano wa siku mbili unaonza hii leo kujadili mustakabali wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu iliyo na makao yake mjini Strasbourg. Mahakama hiyo ya Ulaya iliyoundwa mwaka 1959, chini ya msingi wa mkataba wa haki za binadamu, ni taasisi aina ya kipekee na sasa imekuwa muhanga wa ufanisi wake mkuu. Kwani zaidi ya raia 200,000 kutoka jumla ya wakaazi milioni 800 wa nchi wanachama 47 wa Baraza la Ulaya,wamekuwa wakiitumia mahakama hiyo walipohisi kuwa uamuzi fulani wa serikali ya kitaifa umekwenda kinyume na haki zao za kimsingi. Rais wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu, Mfaransa Jean Paul Costa, amependekeza kufanywe mageuzi yatakayosaidia kupunguza mzigo wa mahakama hiyo, lakini bila ya washtaki kupoteza haki zao za kimsingi. Tangu mwaka 2007 rais wa zamani wa mahakama hiyo, Luzius Wildhaber kutoka Uswisi, alijaribu kuwapunguzia kazi majaji 17 wa mahakama hiyo mjini Strasbourg. Amesema: "Tumejaribu miaka yote niliyokuwepo, kurahisisha utaratibu wa kusikilizwa kesi. Tumeondowa pia mambo tofauti ambayo pengine peke yetu tusingeweza kuyaondowa. Kutokana na umuhimu wa hali ya mambo iliyokuwepo,tumepanga kwa mfano malalamiko ambayo kwa maoni yetu tulihisi si ya kimsingi, yakataliwe kwa njia ya barua tu bila ya kuhitaji ufafanuzi mrefu. Zamani ufafanuzi timamu ulihitajika."
Luzius Wildhaber, Präsident EU Menschenrechtsgerichtshofs
Rais wa zamani wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu, Luzius Wildhaber.Picha: AP
Wildhaber amesema kuwa katika mwaka wake wa mwisho, kama rais wa mahakama hiyo, hadi malalamiko 50,000 yalifikishwa mjini Strasbourg. Zaidi ya asilimia 90 ya hoja hizo zilitupiliwa mbali kwani hazikuwa na sababu, zimetuwama katika sheria ambazo wala hazikutajwa katika mkataba wa mahakama hiyo na pia ilikuwa kazi ya serikali ya nchi ihusika. Licha ya jitahada hizo bado zaidi ya kesi 100,000 zinangojea kuamuliwa katika mahakama hiyo ya Strasbourg na nyingi zinangojea kwa zaidi ya miaka miwili. Leo hii mkutanoni mjini Interlaken, Rais Costa atawasilisha mpango wa mageuzi kuhusu kesi zisizo na msingi na zinazokataliwa. Katika siku zijazo, jaji mwenyewe ataweza kuamua kuhusu kesi za aina hiyo bila ya kwanza kushauriana na baraza mojawapo kati ya mabaraza matatu ya mahakama hiyo. Majadilianio kuhusu mageuzi hayo na hatua zingine za kuimarisha utaratibu wa mahakama hiyo yamekuwa yakifanywa tangu miaka sita iliyopita. Urusi ilikuwa nchi ya mwisho miongoni mwa wanachama 47 kutoa idhini yake mwezi uliopita. Mwandishi: Zumach,Andreas/ZPR/ P.Martin Mhariri Hamidou,Oummilkheir