1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano kuhusu hali ya hewa waanza Bali

Siraj Kalyango3 Desemba 2007

Wajumbe zaidi ya 10,000 kutathmini kupanda kwa hali joto duniani.

https://p.dw.com/p/CW0O
Wajumbe wa mkutano wa hali ya hewa mjini Bali Indonesia.Mkutano huu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa.Picha: AP

Mkutano wa kuhusu kubadilika kwa hali ya hemwa umefunguliwa jumatatu mjini Bali nchini Indonesia kwa lengo la kutafuta njia za kukomesha uchafuzi wa mazingira.Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya elf 10 kutoka nchi 190.Wajumbe kutoka nchi mbali mbali za dunia pamoja na mashirika mbalimbali,mkiwemo wana sayansi, wanasiasa na waandishi habari wanahudhuria mkutano kuhusu kubadilika kwa hali ya hewa.Mkutano huu unasemakena ndio mkubwa zaidi kufanyika kuhusu mada hiyo.

Wakati wa kikao cha ufunguzi washiriki wameombwa kutafuta kwa haraka muafaka wa kimataifa ifikapo mwaka wa 2009, la sivyo dunia itakabiliwa na majanga sio tu ya kimazingira lakini pia ya kiuchumi chanzo kikiwa kuongezeka kupanda kwa hali joto.

Akihutubia kikao cha ufunguzi, anaehusika na mkutano kuhusu hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa, Yvo de Boer amesema kuwa ni muhimu kujifunza na yaliyotokea wakati wa nyuma.

'...tunaweza kujifunza kutoka miaka miwili iliopita kuwa mdahalo, sanasana kuhusu suala nyeti kama hili, ni muafaka kwa majadiliano sawa. Nataraji kuwa kutapatikana suluhu hapa Bali kupitia upasishwaji wa ajenda.Najua kuwa mtaikabili vilivyo changamoto mliopewa na wanasiasa viongozi kadhaa pamoja na wanasayansi mbalimbali.Jukumu mlionalo ni kubwa,' amesema de Boer.

Jukumu walilo nalo ni kuwa mwaka huu kumetolewa ripoti kadhaa zikisema kuwa, hali ya joto inazidi kuongezaka, na pia kuwa teknolojia ipo ya kupunguza kasi ya hali joto duniani.Lakini jambo muhimu ni kuchapuza kuweka vitendoni mbinu za kupunguza kasi ya hali joto.

Shabaha ya haraka ya mkutano wa Bali, utakao dumu wiki mbili ni kuzindua mdahalo kuelekea kuweka mkataba mwingine utakaochukua ule wa Kyoto wa kuhusu ujoto duniani. Mkataba wa Kyoto unamalizika mwishoni mwa mwaka wa 2012.

Kupanda kwa ujoto duniani kumesababisha viwango vya maji ya bahari kupata kupita kiasi, na hivyo kuwafanya mamilioni ya watu kuwa maskani na pia kuwafanya wanyama wengi kutoweka.Wajumbe katika mkutano wa Bali watajaribu kutathmini ikiwa kupunguza kutoa gesi ya kaboni kuwe kwa hiari ama karaha.Pia njia za kusaidia nchi maskini kutoharibu misitu zitajadiliwa.