1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkosoaji wa Uislamu aomba msaada wa ulinzi

15 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D7o1

BRUSSELS:

Mbunge wa zamani wa Uholanzi anaekabiliwa na vitisho vya kuuliwa kwa sababu ya kuikosoa dini ya Kiislamu,ametoa mwito kwa Umoja wa Ulaya kumlipia gharama za ulinzi na hata wengine walio katika hali kama yake.Mzaliwa wa Somalia Ayaan Hirsi Ali alikuwepo mjini Brussels siku ya Alkhamisi kuomba msaada wa Euro milioni mbili kuwalipa walinzi wake.Baada ya kuuawa kwa mtengeneza filamu wa kiholanzi,Theo Van Gogh katika mwaka 2004,Hirsi Ali aliishi chini ya ulinzi mkali wa polisi.Sasa anaishi Marekani na anapaswa kujilipia gharama za ulinzi wake.