1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Liz Cheney ashindwa kwenye kura za mchujo

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
17 Agosti 2022

Liz Cheney, mkosoaji wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na mbunge wa Wyoming, ameshindwa kwenye kura za mchujo za chama cha Republican za kuwachagua wajumbe watakaogombea kwenye uchaguzi mkuu.

https://p.dw.com/p/4FeGO
USA Wahl Wyoming | Liz Cheney
Picha: Jae C. Hong/AP/picture alliance

Liz Cheney mwakilishi wa jiji la Wyoming lililo katika eneo la Kent, jimboni Michigan na mkosoaji mkubwa wa Donald Trump, amepoteza nafasi ya kugombea tena kiti chake cha bunge kwa mgombea anayeungwa mkono na Trump, Harriet Hageman katika kura ya mchujo ya chama hicho cha Republican hapo jana Jumanne.

Ushindi wa Harriet Hageman unadhihirisha jinsi Donald Trump alivyo na ushawishi mkubwa ndani ya chama cha Republican na wakati huo huo ushindi huo unaonesha mafanikio katika kampeni ya Trump ya kuwaondoa Warepublican waliounga mkono zoezi la kumtimua madarakani baada yakutokea ghasia za Januari 6, mwaka 2021 katika bunge la Marekani.

Harriet Hageman aliyemshinda Liz Cheney katika kura za mchujo kwenye eneo la Wyoming.
Harriet Hageman aliyemshinda Liz Cheney katika kura za mchujo kwenye eneo la Wyoming.Picha: Mead Gruver/AP Photo/picture alliance

Cheney, mbunge anayewakilisha eneo la Wyoming kwa awamu tatu sasa ni mmoja kati ya wawakilishi wawili wa chama cha Republican waliomo kwenye jopo la Bunge linalochunguza vurugu zilizotokea katika Bunge la Marekani zilizofanywa na kundi la wafuasi wa Donald Trump.

Katika hotuba yake ya kukubali kushindwa, Liz Cheney amesema amempigia simu Harriet Hageman kumpongeza na kwamba kura hii ya mchujo imemalizika lakini sasa kazi halisi ndio inaanza. Cheney pia alidokeza juu ya mustakabali wake kisiasa ambapo amesema anatarajia kugombea nafasi ya juu zaidi ambayo ni kinyang'anyiro cha urais ifikapo mwaka 2024, kwa maana kwamba huenda akashindana na Donald Trump.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Drew Angerer/Getty Images

Liz Cheney alishinda uchaguzi wa bunge kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2016 na kisha mwaka 2018 na pia mwaka 2020. Baba yake, Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Dick Cheney, alishikilia kiti hicho hicho kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1989. Muhula wake wa tatu na wa mwisho unamalizika Januari mwakani. Ataendelea kuliongoza jopo inalochunguza mashambulizi ya Januari 6 hadi litakapovunjwa mwishoni mwa mwaka huu.

Vyanzo:/AP/ https://p.dw.com/p/4FdBO