1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkopo kwa Ugiriki bado uko mbali

10 Februari 2012

Mataifa ya eneo la euro yanataka kuendelea kutoa msaada kwa Ugiriki lakini kwanza ni pale tu nchi hiyo ambayo imezongwa na madeni itakapopiga hatua ya kutimiza masharti yote yanayotakiwa na Umoja wa Mataifa ya Euro.

https://p.dw.com/p/141EG
Luxembourg's Finance Minister Jean Claude Juncker, left, talks to European Commissioner for Economic and Monetary Affairs Olli Rehn, prior to the start of the Eurogroup ministerial meeting at the European Council building in Brussels, Thursday, Feb. 9, 2012. Germany's finance minister says a deal between Greek party leaders on new spending cuts appears to not yet fulfill all the conditions for a eur 130 billion ($173 billion) bailout. (Foto:Yves Logghe/AP/dapd) na
Waziri wa fedha wa Luxembourg Jean Claude Juncker kushoto na kamishna wa EU wa masuala ya fedha Olli RehnPicha: dapd

Makubaliano yaliyofikiwa na vyama vinavyounda serikali ya mseto nchini Ugiriki ya kubana zaidi matumizi na kupunguza wafanyakazi hayakufikia katika kiwango cha kuwaridhisha mawaziri wa fedha, kama yanavyoeleza matokeo ya mkutano wa mawaziri wa kundi hilo jana jioni mjini Brussels.

Serikali ya Ugiriki imeliweka kundi la mataifa ya umoja wa sarafu ya euro katika hali ya majaribu makubwa. Kila wakati majadiliano juu ya hatua mpya za kubana matumizi yamekuwa yakikwama mahali fulani ama baadhi ya viongozi wa vyama wamekuwa wakipinga hili ama lile.

Ni muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa kikao cha mjini Brussels ndipo taarifa zilizoleta ahueni zikawasili: Ugiriki inasema ndio kwa mpango mpya wa kubana matumizi, na hatua za mageuzi. Waziri wa fedha wa Ugiriki, Evangelos Venizelos, akasema kwa kujiamini wakati alipowasili mjini Brussels kuwa mjini Athens, viongozi wamekubaliana kuhusu mpango mpya wa wadai na wa hatua kali zaidi.

Mpira sasa uko upande wa mataifa ya umoja wa sarafu ya euro.

"Tunahitaji sasa idhinisho la kisiasa la mataifa ya sarafu ya euro ili kufikia hatua ya mwisho."

Watumishi wachache wa serikali, kupunguza mishahara, na hasa suala linaloleta mivutano, la kupunguza mafao ya malipo ya uzeeni pamoja na kupunguza kiwango cha chini cha mshahara, hizi zote ni maada zilizomo katika dawa chungu ambayo vyama vinavyounda serikali ya mseto nchini Ugiriki ilibidi kumeza.

Hata hivyo hayo yote hayakutosha kuwaridhisha mawaziri wa fedha wa mataifa ya eneo la euro. Waziri wa fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schäuble, aliliona hilo hata kabla ya mkutano kuanza.

epa03098277 German Finance Minister Wolfgang Schaeuble arrives for a European Finance Ministers Meeting on Greece at the European Council headquarters in Brussels, Belgium, 09 February 2012. Eurozone finance ministers were due to discuss a second bailout package for Greece over dinner, hours after the government in Athens agreed to adopt harsh new austerity measures and struck a debt write-off deal with private creditors. 'Negotiations with representatives of the European Union, the International Monetary Fund (IMF) and the European Central Bank (ECB) have been successfully concluded,' Greek Prime Minister Lucas Papademos said in Athens. EPA/OLIVIER HOSLET +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang SchäublePicha: picture-alliance/dpa

"Majadiliano yamepiga hatua kubwa, lakini hatujafika mbali, na ni vizuri, kwamba tunapata matokeo ya mwanzo na kwamba sisi pamoja na Ugiriki na washirika wa mazungumzo haya wakaiambia wazi Ugiriki, kile tunachokihitaji ili kupata makubaliano ya pili na Ugiriki. Tutaonana tena, pale majadiliano nchini Ugiriki yatakapopata mafanikio na pale kundi la pande tatu litakapofikia makubaliano."

Mambo matatu lazima

Ilipofika usiku wa manane mkuu wa kundi la mataifa ya euro Jean-Claude Juncker alijitokeza mbele ya waandishi habari na kuthibitisha yale aliyokuwa akifikiria waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble. Hakuna malipo bila ya kupata matokeo kamili, ndivyo alivyofupisha mawazo ya mkutano huo wa mawaziri. Kwa jumla alitaka mambo matatu yafanyike.

"Kwanza ni lazima bunge la Ugiriki siku ya Jumapili kuidhinisha hatua za mpango uliokubaliwa kati ya Ugiriki na kundi la pande tatu. Pili ni lazima kuendelea na hatua za kufanyia mageuzi hatua za kupunguza matumizi ya euro milioni 325 kwa mwaka huu wa 2012 haraka, ili kuweza kupata uhakika, kwamba inawezekana kufikia lengo la kupunguza nakisi. Na tatu tunataka hatua imara za kisiasa kutoka kwa mkuu wa serikali ya mseto ili kuweza kutekeleza mipango hii."

EU-Finanzgipfel gescheitert Luxembourg's Prime Minister and President of the European Council Jean Claude Juncker gestures during a news conference at the end of the European Head of States council at Brussels Friday 17 June 2005. EU leaders were facing a bruising clash over the bloc's long-tem budget on Friday, with Britain steadfastly defending its cherished rebate in the teeth of opposition from its 24 fellow member states. EPA/OLIVER HOSLET +++(c) dpa - Report+++
Mkuu wa nchi za sarafu ya euro Jean Claude Juncker,Picha: dpa

Hata hivyo hali hiyo si rahisi kama inavyoonekana. Katika miji mikuu ya mataifa hayo ya eneo la euro kuna hali ya uwazi kuhusu chochote kitakachotokea. Kwa muda wa siku chache zilizopita kamishna wa umoja wa Ulaya, Neelie Kroes, alivunja tabia ya ukimya. Kwa hali yoyote ile iwayo ni lazima Ugiriki iwekewe mbinyo. Ni lazima serikali ya Ugiriki kwa hali yoyote ile ionyeshe kuwa inafanya kitu, kabla ya kupewa fedha zaidi.

Mwandishi: Christopher, Hasselbach/ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo