1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkenya ahukumiwa kwa kumuiga rais kuwatapeli watu

Sekione Kitojo Yusuf Saumu
27 Februari 2019

Watu 7 waliojifanya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kuwatapeli wafanyabiashara kiasi cha shilingi milioni 10 wameshitakiwa nchini Kenya.

https://p.dw.com/p/3EBYa
Kenia Uhuru Kenyatta
Picha: imago/i Images

Mahakama nchini Kenya imewashitaki watu saba kwa kujifanya kuwa ni rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo na kujipatia fedha  kutoka kwa mfanyabiashara maarufu kiasi cha shilingi za Kenya milioni 10, sawa na dola laki moja katika kesi kubwa ya rushwa.

Watuhumiwa walimpigia mkuu wa kampuni ya matairi ya Sameer Africa Naushad Merali na mkurugenzi wake wa fedha Akif Butt wakijifanya ni rais anayetaka kuwauzia ardhi, nyaraka za mahakama zilionesha.

Watu hao wamedai hawana hatia katika mahakama ya mjini Nairobi na wameachiliwa huru kwa dhamana kabla ya kesi yao kuanza  tena Machi 12.

Mmoja kati ya watu hao aliiga sauti ya rais Kenyatta, wakati wengine waliwasili katika magari ya kifahari na suti kuchukua fedha hizo, polisi imesema.

Nyaraka za mahakama zimeeleza kwamba Merali alitoa kibali kwa mkurugenzi wa fedha kufanya malipo akiamini kwamba alikuwa akizungumza na kiongozi wa taifa hilo.