1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa usalama baina ya Iraq na Marekani

Miraji Othman28 Novemba 2008

Majeshi ya Marekani yatabakia Iraq hadi mwisho wa mwaka 2011

https://p.dw.com/p/G417
Waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki(kushoto), akizungumza na mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali KhameneiPicha: AP

Jana alhamisi bunge la Iraq liliukubali mkataba wa usalama baina ya nchi hiyo na Marekani, mkataba ulioleta mabishano ndani ya k Iraq kwenyewe. Kwa wingi wa kura, bune liliyakubali mapatano hayo yanayotaja kuondoka majeshi ya Kimarekani kutoka nchi hiyo ifikapo mwisho wa mwaka 2011. Upigaji wa kura kwanza ulipangwa ufanyike jumatano iliopita, lakini ukaahirishwa hadi jana kutokana na mabishano baina ya serekali na upande wa upinzani. Uongozi wa kisiasa pamoja na shehe wa madhehebu ya Shia aliye na ushawishi mkubwa, Ali al-Sistani, hapo mwanzo walitaka mkataba huo ukubaliwe na watu wengi wa makundi ya kisiasa na ya kidini. Lakini: jee mkataba huo utaipatia Iraq utulivu unaotumaniwa?

Ilichukuwa miezi mingi ya mashauriano makali baina ya serekali ya Iraq na ile ya Marekani hadi ukapatikana mkataba huu ambao unataja juu ya msingi wa kisheria wa kuweko majeshi ya Kimarekani katika Iraq. Hata hivyo, wabunge wa Iraq walitakiwa kwanza waukubali mkataba huo. Huenda waziri mkuu, Nour al-Maliki, na wafuasi wake pamoja na washirika wake wa Kikurd walikuwa na wingi bungeni, hata hivyo, alitaka mkataba huo uungwe mkono na watu wengi zaidi ili auimarishe msimamo wake. Ilivikuwa sasa amelifikia lengo hilo, suali linabakia kama mkataba huo kweli utaituliza Iraq, hasa ilivokuwa mwisho wa nchi hiyo kukaliwa na majeshi ya kigeni unakaribia.

Kuna kila sababu ya kutilia ati ati jambo hilo. Kwanza ni kwamba Wamarekani na wa-Iraqi wanauangalia mkataba huo kwa mitizamo tafauti. Kwa Marekani, mkataba huo juu ya majeshi yake ni sawa na ile mikataba thamanini ambayo Marekani imetiliana saini na nchi mbali mbali duniani juu ya uhalali wa kisheria wa kuweko majeshi hayo katika nchi hizo. Na kwa Iraqi, mkataba huo ni hatua ya kwanza ya kuondoka majeshi hayo kutoka nchi hiyo ya Kiarabu. Mwakani majeshi ya Kimarekani yatatakiwa yaondoke kutoka mijini, na hadi mwisho wa mwaka 2011 yaondoka kabisa kutoka Iraq.

Karatasini mambo hayo yanaonekana kuwa ni mazuri, lakini kama kweli hayo yaliokubaliwa yatatekelezwa, hamna mtu anayejuwa. Mtu haifai kusema kwamba Wamarekani wana nia mbaya, lakini miaka mitatu ni muda mrefu na mambo mengi yanaweza yakatokea. Pindi hali ya usalama huko Iraq itazidi kuwa mbaya, basi Rais mteule Barack Obama huko washington atakuwa katika mtihani, kama majeshi ya Kimarekani yatabidi yaondoke nchini hata kabla ya mambo hayajatulia na kurejea kuwa ya kawaida. Kuondoka kwa namna hiyo kutatafsiriwa moja kwa moja kuwa ni kushindwa Marekani, na Barack Obama hatalikubali jambo kama hilo, kwa urahisi.

Na pia, kwa upande wa serekali ya Iraq kuna hamu kubwa kwamba nchi hiyo, kutokana na kuondoka majeshi ya Kimarekani, isirejee tena katika michafuko, kama ilivokuwa katika miaka iliopita.

Lakini vipi itakuwa pindi wavamizi wa Kimarekani watakabidhi madaraka kwa serekali ya Baghdad pia bila ya kuweko mikwaruzano? Bado kuna wasiwasi kwamba sura itakayojitokeza ni kama vile Marekani inaondoka Iraq na haijasababisha kufariki watu wengi, hasa kwa upande wa Iraq; sura itakayojitokeza ni kama vile hamna kitu kilichojiri. Wale maafisa wa Kimarekani waliokuwa na ushawishi katika siku za zamani za utawala wa Clinton watakwenda mbio kuona kwamba wanazielewa thamani za kijeshi na za kiuchumi za Iraq itakayokuwa na amani na pia kuwa karibu na Marekani. Serekali ya Rais Bush, ambayo ndio iliouandaa mkataba huu wa amani, kwa vyovyote, haijafikiria juu ya kuondoka majeshi ya Kimarekani kutoka Iraq ifikapo mwaka 2011, ama sivyo isingejenga vituo vya kijeshi vingi na vya gharama katika nchi hiyo kama ilivofanya mwaka uliopita.

Lakini katika miaka mitatu mambo mengi yanaweza yakatokea; na huenda mambo hayo yakawa mazuri. Mtu atarajie kwamba kwa kuukubali mkataba huo wa amani, Wa-Iraq hawatafungua tu ukurasa, lakini mlango mpya wa historia ya kutisha ya miaka iliopita.