1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa Kyoto wapata uhai

9 Desemba 2012

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi jana Jumamosi08.12.2012)umerefusha uhai wa mkataba wa Kyoto,ambao ndio pekee unaolazimisha mataifa kupunguza utoaji wa gesi chafu,ukiwa ushindi mdogo na muhimu.

https://p.dw.com/p/16ygH
epa03489061 European Climate Action Commissioner Connie Hedegaard speaks during a news conference on the upcoming international climate negotiations in Doha, at the European Commission headquarters, in Brussels, Belgium, 28 November 2012. The 18th global climate change conference opened in Qatar on 26 November 2012 with representatives from nearly 200 nations convening for two weeks of talks aimed at curbing global carbon emissions. EPA/JULIEN WARNAND +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mkutano wa Doha wa mazingira ukiendeleaPicha: picture-alliance/dpa

Ilichukua majadiliano marefu na saa kadha bila kupata usingizi katika mji mkuu wa Qatar, Doha hadi yalipofikiwa makubaliano kuhusu hatua za mpito kuzuwia mabadiliko ya tabia nchi, yakisubiriwa makubaliano mapya ya dunia ambayo yataanza kufanyakazi mwaka 2020.

Urefushwaji wa mkataba wa Kyoto uliidhinishwa hatimaye na mataifa ya umoja wa Ulaya, Australia, Uswisi na mataifa manane mengine yenye utajiri mkubwa wa viwanda yakitia saini upunguzaji wa lazima wa utoaji wa gesi za viwandani ifikapo mwaka 2020.

Mataifa hayo yanawakilisha utoaji wa asilimia 15 wa gesi chafu zinazoharibu mazingira duniani. Kiongozi wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameyakaribisha makubaliano hayo, ambayo yanatambulika kama lango la Doha katika mazingira, kuwa ni hatua ya kwanza muhimu lakini amesema kwa kupitia msemaji wake kuwa , "hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa."

Local and international activists march inside a conferences center to demand urgent action to address climate change at the U.N. climate talks in Doha, Qatar, Friday, Dec.7, 2012. A dispute over money clouded U.N. climate talks Friday, as rich and poor countries sparred over funds meant to help the developing world cover the rising costs of mitigating global warming and adapting to it. (Foto:Osama Faisal/AP/dapd)
Maandamano hayakukosa mjini DohaPicha: dapd

Mataifa tajiri yabanwa

Makubaliano hayo yanayafunga tu mataifa yaliyoendelea, yakiweka kando mataifa makubwa yanayoendelea yanayochafua zaidi mazingira kama vile China na India, pamoja na Marekani ambayo inakataa kuidhinisha mkataba wa Kyoto.

Kimsingi, wataalamu wamesema kuwa kurefushwa kwa mkataba huo kutaleta tofauti kidogo tu kwa viwango vya uchafuzi wa mazingira kwa kuwa unajumuisha sehemu ndogo ya utoaji wa gesi hizo chafu na mataifa yaliyotia saini yana malengo yake yaliyopitishwa kisheria hata hivyo.

"Ni hatua ndogo lakini muhimu kuelekea mbele," kamishna wa masuala ya mazingira wa umoja wa Ulaya Connie Hegegaard amesema mwishoni mwa mazungumzo hayo ambayo yaliendelea siku nzima ya Ijumaa hadi usiku na kuingia katika siku nzima ya muda wa nyongeza, wakati nchi tajiri na masikini zikipambana kuhusiana na utoaji wa fedha na fidia kwa ajili ya madhara yaliyopatikana kwa mazingira.

Baada ya siku 12 za mvutano ambao ulionekana kushindwa tangu mwanzoni, mwenyekiti wa mkutano huo Abdullah bin Hamad al-Attiyah hatimaye aliharakisha kupitishwa kwa makubaliano hayo jioni ya Jumamosi(08.12.2012).

Qatar's Deputy Prime Minister and 18th Conference of the Parties (COP18) President Abdullah bin Hamad Al-Attiyah speaks at the opening session of the United Nations Climate Change (COP18) Conference in Doha November 26, 2012. REUTERS/Fadi Al-Assaad (QATAR - Tags: POLITICS ENVIRONMENT HEADSHOT)
Rais wa mkutano huo wa umoja wa mataifa Abdullah bin Hamad Al-AttiyahPicha: Reuters

Hapo kabla aliwahimiza wajumbe kupata muafaka na "sio kuanzisha majadiliano ambayo hayana mwisho tena kwa sababu hatutamaliza", onyo ambalo hata hivyo lilipuuziwa.

Atumia rungu

Attiyah alilazimika kusubiri katika ukumbi kwa zaidi ya saa nne wakati mapambano yakiendelea. Makamu waziri mkuu huyo alizuwia mapambano zaidi kutokana na kupinga kwa baadhi ya mataifa wakati akipiga rungu lake kila mara na huku akitoa tamko: "Imeamuliwa hivi" huku akishangiliwa kwa nguvu.

Urusi ilitoa pingamizi la kupitishwa kwa makubaliano ya Kyoto, ambayo awamu yake ya kwanza inamalizika Desemba 31.

Duru ya hivi sasa ya mazungumzo ya mabadiliko ya tabia nchi ya Umoja wa Mataifa, ambayo imeonekana kuburuza miguu mno wakati wajumbe wa majadiliano wakibishana hadi dakika za mwisho kama vile katika mchezo wa karata na kujaribu kuvicha karata zao, wakishindwa kupata uvumbuzi kuhusu utoaji wa fedha pamoja na mikopo ya hewa chafu.

Biashara ya gesi chafu

Hewa chafu ina maana ya biashara ya utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira, viwango ambavyo nchi ziliruhusiwa kutoa katika mkataba wa Kyoto wa mwaka 1997 na havikufikiwa, ikiwa ni kiasi cha tani bilioni 13 za gesi hizo kwa jumla.

Poland na Urusi bado zina kiwango hicho cha mkopo, kwa kuwa zilitoa gesi chafu cache zaidi kuliko viwango inavyoruhusiwa, na zinasisitiza kuwa ziruhusiwe kuhifadhi tofauti iliyopo kupindukia mwaka 2012, hatua ambayo makundi mengine yanapinga kwa nguvu zote.

Marcin Korolec, polnischer Umweltminister auf dem Klimagipfel in Doha *** aufgenommen am 5.12.2012 in Doha, Qatar Deutsche Welle, Andrea Rönsberg
Waziri wa mazingira wa Poland Marcin KorolecPicha: DW/A. Rönsberg

Makubaliano hayo hayaruhusu mikopo ihifadhiwe, lakini masoko muhimu, ikiwa ni pamoja na umoja wa Ulaya , Australia na Japan , imeelezwa katika waraka huo kuwa hazitaruhusiwa kununua.

Mataifa yaliyoendelea yalikuwa katika mbinyo mjini Doha kuonyesha vipi yanataka kuweka ahadi yao ya kuongeza fedha kwa ajili ya mazingira kwa nchi masikini kufikia dola bilioni 100 kila mwaka ifikapo mwaka 2020, kutoka idadi ya jumla ya dola bilioni 30 katika mwaka 2010 hadi 2012.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / dpae

Mhariri: Iddi Ssessanga