1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkasa wa mshindi wa Tour de France -van Niestelroy aenda Real

Ramadhan Ali28 Julai 2006

Al ahly,mabingwa wa Afrika wanarudi uwanjani kutetea taji lao huku Beni McCathy akihamia Blackburn Rovers kutoka FC Porto.Ligi ya Ufaransa imeanza.

https://p.dw.com/p/CHdT

Mwishoni mwa wiki hii,likizo zilizofuatia Kombe la dunia zimemalizika kwa baadhi ya viwanja vya dimba wakati kwengineko zinaendelea.

Ujerumani inacheza kunaaniwa leo Kombe la Ligi la ujerumani linalotangulia kuanza kwa msimu mpya wa Bundesliga.

Jioni hii basi, Hamburg ina miadi na Hertha Berlin wakati Schalke inakumbana na Bayer Leverkusen katika robo-finali ya kombe hilo la ligi.

Ligi ya Ufaransa talari imeanza ijumaa na inaendelea , kesho Olympique Lyon inamenyana na Paris St.Germain na huko Amerika kusini ni zamu ya nusu-finali ya Libertadores Cup –kombe la klabu bingwa za America Kusini hapo jumatano na alhamisi.

Jogoo la Manchester united, ruud van Nistelrooy limefunga mkataba na Real madri dna sio Bayern Munich kwa msimu ujao.

Kwa kitita cha Euro milioni 15, Real imemkomboa van Niestelrooy kutoka Manchester na kufungisha mkataba wa miaka 3.van Niestelrooy atakua mchezaji 3 wiki hii kuajiriwa na Real madrid baada ya kumtia mfukoni nahodha wa Itali Fabio Cannavaro na Mbrazil Emerson.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech,Pavel Nedved ameamua kuzama daraja ya pili na klabu yake ya Juventus ya Itali badala ya kuwafuata wachezaji wengine kama Emerson,Cannavaro na Lilian Thuram pamoja na Zambrotta kujiunga na timu n yengine.

Nedved alichaguliwa mchezaji bora wa dimba wa mwaka wa Ulaya 2003.Ameungama kuwa ametakiwa ajiunge na klabu nyengine lakini moyo wake bado unapiga Juventus.

Juventus imeteremshwa daraja ya pili kama adhabu ya kupangilia matokeo na kuwahonga marifu.

Hata stadi wa Afrika Kusini –Benni McCathy ,anaihama klabu yake alioibuka nayo mabingwa wa Ulaya-FC Porto.

Benni ataichezea Blackburn Rovers ya uingereza msimu ujao.McCarthy mwenye umri wa miaka 28 alichangia mno kuitawaza Porto mabingwa wa Ulaya 2004 na amekuwa akiandaa mpango wa kuhamia Premier League-Ligi ya uingereza tangu pale kocha wake wa zamani Jose Mourinho kuchukua uongozi wa Chelsea.

Duru nyengine ya kombe la klabu bingwa barani Afrika iko uwanjani jumamosi hii:Katika kundi A, Asante kotoko ya Ghana inumana na CS Sfaxien ya Tunisia .Mabingwa Al Ahli ya Misri wana miadi na JS Kabylie ya Algeria.

Jumapili itakua zamu ya kundi B: Mabingwa wa zamani Enyimba wa Nigeria wanaumana na Orlando Piarates ya Africa Kusini wakati ASEC Mimosas ya Ivory Coast ina miadi na Hearts of Oak ya Ghana.

Al Ahly mabingwa wakiumana na Kabylie mjini Cairo hi ileo jioni ,itabidi kucheza bila ya beki wao mshahara Emad al-Nahas pamoja na mshambulizi Emad Moteab.

Hatahivyo, Al Ahly wanatazamiwa kutamba nyumbani leo kwani hawataregeza tena kamba kwavile wanataka kutwaa Kombe hili kwa mara ya tatu na kuweka rekodi walioshindwa kuiweka Enyimba.

Sawa na Al Ahly, Asante kotoko ya Ghana inahitaji pointi zote 3 katika zahama yao na Sfaxien ya Tunisia .Sfaxien iliitoa Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na FAR Rabat ya Morocco.

Enyimba ndio timu pekee ilioshinda ugenini katika duru ya kwanza walipoichapa Hearts of Oak ya Ghana mabao 2:0.ASEC ilitia bao dakika za kufidia kuondoka suluhu na Orlando Pirates ya Afrika Kusini mjini Johannesberg.

Tukibakia Johannesberg,wakuu wa ringi ya mabondia nchini Afrika Kusini wanafanya juhudi kubwa kumvutia mbondia wa kike Leila Ali-mwana wa mbabe wa zamani Muhammad Ali kurejea Afrika Kusini baada ya mpam,bano uliopangwa kabla kuvunjwa.Leila akarejea Marekani mapema wiki hii huku pakiwepo mabishano kati yak ambi yake na waandazi –Sta-Trade.

Hii ilitokana na kushindwa kwa Sta-Trade kujipatia fedha za kutosha kugharimia changamoto hiyo ya August 5 kati ya Leila na Gwendolyn O`Neil wa Guyana mjini Cape Town.

Mwishoe, mkasa wa madhambi ya doping-matumizi ya madawa kutunisha misuli umeibuka tena kuhusu mbio za baiskeli za Tour de France.

Mshindi wa wiki iliopita muamerika Floyd Landis amegunduliwa alitumia madawa .Binafsi Landis anakanusha na hivyo matokeo ya uchunguzi wapili yanangonjewa kwa hamu.

Endapo uchunguzi wa pili ukithibitisha tena,basi mbio za baiskeli za Tour de France zitazidi kuwa mashakani.Kwani hii si mara ya kwanza kwa Tour de France kukumbwa na kashfa kama hii.

Mshindi wa mara iliopita Lance Armstrong alituhumiwa pia kufanya madhambi hayo na mjerumani Jan Ulrich,alitolewa katika mashindano ya mwaka huu kutokana na tuhuma kama hizo.Na kama kawaida watuhumiwa daima wanakataa madhambi yao.

Kwa kituo cha Tv cha Ujerumani-ZDF-maji sasa yamezidi unga.ZDF imetangaza kwamba inazingatia kutoonesha tena mashindano haya kufuatia kisa hiki kipya cha mshindi-bandia .

ZDF imenukuliwa kusema, “Imefunga mkataba kuonesha mashindano ya kispoti na sio mashindano ya kampuni gani la madawa lina dawa mujarubu zaidi ya kufanya madhambi ya doping kuliko mwenziwe.”