1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan ajiuzulu

14 Septemba 2023

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan amejiuzulu jana Jumatano, kwenye hotuba yake ya mwisho mbele ya Baraza la Usalama la Umoja huo.

https://p.dw.com/p/4WKov
Aliekuwa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes
Aliekuwa Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker PerthesPicha: Alessandro Della Valle/KEYSTONE/dpa

Mjumbe huyo alionya kwamba mzozo kati ya viongozi wa majeshi yanayokinzana nchini humo unaweza kubadilika na kuwa vita kamili. 

Volker Perthes, ambaye utawala wa kijeshi wa Sudan ulimzuia kuingia nchini humo, amekuwa akiendeleza shughuli zake nje ya Sudan, amesema mapigano nchini humo hayaonyeshi dalili ya kumalizika, wakati pande zote zikionekana kutokuukaribia ushindi.

Soma zaidi: Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya Sudan Ajiuzulu

Amezungumzia pia machafuko katika jimbo la Darfur ambayo amesema yameongezeka sana, wakati walengwa wakubwa wakiwa ni raia kwa kuzingatia makabila. 

Mjumbe huyo aidha amesema kumepatikana makaburi karibu 13ya halaiki ndani na katika eneo la mji mkuu wa jimbo la  Darfur Magharibi  wa Geneina. Jimbo hilo lilikuwa kitovu cha kampeni ya mauaji ya halaiki mapema miaka ya 2000.