Maghorofa marefu na migahawa ya kahawa katika wilaya ya Bole huupa mji wa Addis Ababa taswira ya usasa- lakini wakaazi wengi wa mji huu mkuu wa Ethiopia huhangaika kupata riziki. Mwimbaji wa Jazz Sinishaw anaionyesha DW mji wake na kisha burudani ya Jazz usiku.