Sheria ya msingi ya Ujerumani inaeleza kuwa wanaoandamwa kisiasa wana haki ya kupewa kinga ya ukimbizi. Lakini haki hiyo sasa inawekewa swali huku baadhi ya wanasiasa wakitaka sheria hiyo ifanyiwe marekebisho. OumilKheir anaangazia zaidi katika makala ya Sura ya Ujerumani, mjadala ambao umepamba moto kuhusu sheria ya ukimbizi nchini Ujerumani.