1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

FBI na Posta wachunguza vifurushi baada ya kuvitilia shaka

18 Septemba 2024

Shirika la Upelelezi nchini Marekani, FBI pamoja na Huduma za Posta yanachunguza vifurushi walivyovitilia shaka viliyotumwa ama kupokelewa na maafisa wa uchaguzi kwenye majimbo zaidi ya 10.

https://p.dw.com/p/4kjrD
Logo | Amazon
Picha ya mfano wa kifurushi kama kinavyoonekana baada ya kupigwa picha Chicago, Illinois, nchini Marekani Oktoba 15, 2022Picha: Beata Zawrzel/NurPhoto/picture alliance

Vifurushi vya mwisho vilitumwa kwa maafisa wa uchaguzi wa Kentucky, Massachussets, Missouri na New York. Hata hivyo hakuna taarifa zozote ikiwa vifurushi hivyo vilikuwa na viambata hatari.

Mamlaka za Mississippi ziliripoti juu ya kifurushi kilichopokelewa siku ya Jumatatu, huku ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje, kitengo cha uchaguzi  iliyoko Connecticut nayo ikisema FBI iliwaarifu juu ya kifurushi walichokitilia shaka.

Kitisho hiki cha karibuni kinakuja wakati kura za mapema zikianza kupigwa katika baadhi ya majimbo, miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge, maseneta na ofisi muhimu kote nchini humo.