MigogoroAfrika
Misri yawahifadhi Wasudan milioni 1.2: UN
11 Novemba 2024Matangazo
Ripoti ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, iliyotolewa siku ya Ijumaa imeonesha kwamba takwimu za hivi karibuni kutoka kwa serikali ya Misri zinaonesha kuwa zaidi ya Wasudan milioni 1.2 wametafuta hifadhi nchini humo.
Soma pia: Sudan hali ni mbaya na hakuna ishara ya vita kumalizika
Mmoja kati ya maafisa wanaoshughulikia maswala ya uhusiano wa nje katika shirika la UNHCR nchini Misri, Christine Bishay, amesema kwa sasa Misri inawahifadhi wakimbizi zaidi ya laki tano wa Sudan ambao wamesajiliwa rasmi na shirika la wakimbizi, huku wengine wakisubiri kusajiliwa. Maalfu ya watu wameuawa tangu vilipoanza vita mnamo mwezi Aprili 2023 kati ya majenerali wapinzani nchini Sudan.