1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yachapwa bao 1-0 na Uruguay

Sekione Kitojo
15 Juni 2018

Mchezo  wa  kwanza  hii  leo  katika  siku  ya  pili  ya michuano  ya  kombe  la  dunia kati  ya  Misri  na  Uruguay umemalizika  kwa  ushindi  wa  Uruguay  wa  bao 1-0.

https://p.dw.com/p/2zdlZ
WM 2018 | Russland | Ägypten gegen Uruguay | Tor Gimenez
Picha: Reuters/D. Sagolj

Mchezo  wa  kwanza  hii  leo  katika  siku  ya  pili  ya michuano  ya  kombe  la  dunia kati  ya  Misri  na  Uruguay umemalizika  kwa  ushindi  wa  Uruguay  wa  bao 1-0 lililowekwa  wavuni  katika  dakika  ya  89  ya  mchezo kwa kichwa  na  Jose Gimenez  katika  mchezo  wa  kundi  A.

Mshambuliaji  wa  Misri Mohamed Salah aliachwa  nje  ya uwanja  licha  ya  kocha Hector Cuper  kusema  alikuwa katika  hali  nzuri  kuweza  kucheza  katika  mchezo  huo kutokana  na  maumivu  ya  bega aliyopata  katika  mchezo wa  fainali  ya  Champions League  kati  ya  liverpool  na Real Madrid  mwezi  uliopita. 

Misri  walipambana  kiume lakini Uruguay  walipata  nafasi nzuri  zaidi  ambapo  mshambuliaji  wa  Barcelona  Luis Suarez  alikosa  nafasi  nyingi  za  wazi  na  Edson Cavanni alipiga  mpira uliogonga  nguzo  wa  goli  katika  mpira  wa adhabu. Mchezo  mwingine unaoendelea  hivi  sasa  ni  kati ya  Morocco  dhidi  ya  Iran.

Usiku  kutakuwa  na  pambano  la  kukata  na  shoka wakati  mabingwa  wa  Ulaya Ureno  watapambana  na mabingwa  wa  zamani  Uhispania.