1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri yaandaa mkutano kuhusu Sudan

13 Julai 2023

Misri inajaribu kuyapatanisha makundi yanayozozana nchini Sudan kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa kikanda leo.

https://p.dw.com/p/4TqpM
Ägypten Präsident  Abdel Fattah al-Sisi
Picha: Mandel Ngan/AP/picture alliance

Mkutano huo ni wa karibuni katika msururu wa juhudi za kimataifa za kuzuia mripuko wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongezeka kwa mgogoro wa kibinaadamu.

Serikali ya Misri, ambayo kihistoria ina mahusiano ya karibu na jeshi la Sudan, imewaalika majirani wa Sudan kwa mkutano huo wa kilele leo.

Lengo ni kuepusha uingiliaji wa kigeni na ushawishi katika mapigano yanayoendelea.

Soma zaidi: UN: Watu 87 walikwa katika kaburi la pamoja Darful
Kaburi la pamoja lagunduliwa Darfur

Hayo ni kwa mujibu wa vyanzo viwili vya usalama vya Misri.

Aidha mkutano huo utaanzisha mchakato wa kufikiwa makubaliano ya amani ili kukomesha mapigano.

Wapatanishi wanalenga kukutana na wakuu wa kijeshi wa Sudan pamoja na viongozi wa makabila.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya wanamgambo wa RSF yalizuka katika mji mkuu Khartoum mwezi Aprili na yamesambaa upande wa magharibi kuelekea majimbo tete ya Darfur na Khordofan.