1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri kuwaruhusu mashabiki wa kandanda uwanjani

22 Desemba 2014

Misri itawaruhusu baadhi ya mashabiki kuhudhuria mechi za Ligi Kuu ya kandanda nchini humo kwa mara ya kwanza tangu ilipowapiga marufuku mashabiki kuingia viwanjani baada ya vurugu kali zilizozuka uwanjani 2012.

https://p.dw.com/p/1E8fC
Ägypten - Fußball-Fans feiern vor dem Stadion.
Picha: DW/M. Sailer

Taarifa ya shirikisho la kandanda nchini humo imesema hatua hiyo ya kupiga marufuku itaendelea kutekelezwa katika mechi ya timu zozote mbili kati ya vilabu sita vikuu.

Kutakuwa hata hivyo na idadi fulani itakayoruhusiwa kuhudhuria mechi viwanjani, huku mashabiki 10,000 wakiruhusiwa kuangalia michuano itakayoandaliwa katika viwanja vya Cairo na Alexandria na mashabiki 5,000 katika viwanja vidogo kote nchini humo.

Vilabu vikuu Al-Ahly, Zamalek, Al-Ittihad, Ismaily, Al-Masry na Damanhur vitaendelea kucheza katika viwanja vitupu wakati timu yoyote kati ya hizo sita itacheza. Mashabiki 74 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa wakati vurugu zilizpozuka uwanjani Februari 2012 mjini Port Said, baina ya mashabiki wa timu mwenyeji Al-Masry na Al-Ahly ya Cairo.

Mwandishi. Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri. Gakuba Daniel