Miripuko mbili Algiers yaua watu 24
12 Aprili 2007Miripuko 2 ya mabomu katika mji mkuu wa Algeria, Algiers, hapo jana, imesababisha vifo vya watu 24 na zaidi ya wengine 200 wamejeruhiwa.Kwahivyo hii ndio hujuma kali kabisa kutokea Algeria kwa muda mrefu.Kikundi kilicho na mafungamno na Al Qaeda cha wafuasi wa kiislamu wa Maghreb au Afrika ya kaskazini kimejitwika jukumu la hujuma za jana.
Imekuwa desturi tangu Sepremba 11,2001 shambulio lolote la kigaidi bila ya kujali wapi limetokea dhamana kutwikwa mabegani mwa Osama Bin Laden na mtandao wake wa Al qaeda.
Hivi sasa imekuwa pia desturi kutumia mhuri wa Al Qaeda kwa hujuma yoyote inayofanyika duniani.Na hii ni hivyo hata ingawa mtandao wa Al Qaeda hauna tena shina kuu lake mahala pamoja kwa harakati zake ulimwenguni bali sasa umegawa matawi yake sehemu mbali mbali.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu,matawi hayo ya waislamu wenye itikadi kali wamekuwa wakitamba katika eneo la maghreb la Afrika ya kaskazini.Kuna kundi la Algeria linalojiita “Salafist (GSPC) na linamafungamano na vikundi vya aina hiyo katika nchi jiranmi za Maghreb-Morocco,Mauritania na Tunisia.Vikundi vyote hivi vimejiweka sasa chini ya paa moja linalojiita “Jumuiya ya Al Qaeda inayopigania uislamu katika Maghreb.”
Shabaha hii hatahivyo, si mpya:Mnamo miaka ya 1990 vilijaribu vikundi mbali mbali vya kiislamu vyenye siasa kali kupigana na utawala wa Algeria baada ya kuhisi vimefanyiwa ukhaini kwa ushindi wao katika uchaguzi wa 1992.
Shina la wapiganaji hao ni lile la wakombozi wa Afghanistan ambao walijitolea kupigana huko Hindukusch dhidi ya majeshi ya Urusi yaliokalia wakati ule Afghanistan na wakihisi sasa wangeweza kutimiza shabaha kama ile kwao Algeria.
Afghanistan ni beji tu ilioshikamana na Osama Bin Laden na Al Qaeda.Sababu za vita lakini zilikuwa za hali ya ndani nchini zilizofungamana na nadharia ya kiislamu.Nyengine ni umasikini na kutokuwepo mustakbala mwema na hasa kwa chipukizi,lakini pia mkandamizo wa utawala na kushirikiana mno na dola zilizoitwa za makafiri:Marekani na Ufaransa.
Rais Abdelaziz Bouteflika alijaribu kumpunga shetani alipowanyoshea wapiganaji wakiislamu msamaha.Katika msamaha huo lakini walitengwa wamwagaji damu mashuhuri na kwahivyo wasalafist wakaukataay.Kikosi chao cha wapiganaji mia kadhaa kikaapa kuendelea na vita na kukajitanua hadi nchi jirani ambako hali duni sawa na zile za Algeria zimeenea-ufukara na umasikini.
Kueleza kuwa hujuma za jana mjini Algiers, ni ushahidi kwamba juhudi za suluhu zimeshindwa si sawa.Wingi mkubwa wa waalgeria ungependa kuishi katika hali ya utulivu na amani.Walichoshwa na vifo vya waalgeria laki 2.Watu lakini wanataka kuishi kidogo maisha bora na yenye neema .
Na kwa kadiri hawatatimiziwa matumaini hayo, wafuasi wenye siasa na itikkadi kali watapata nguvu.Na ghadhabu zao hazitalengwa tu kwa watawala wao bali pia kwa marafiki na washirika wao mbali na bahari ya Meditteranian au ya Atlantik.