MINSK: Belarus yaongeza kodi ya mafuta ya Urusi
4 Januari 2007Matangazo
Belarus imeongeza kodi inayotoza mafuta ya Urusi yanayopitia ardhi yake huku mzozo wa bei ya nishati ukiendelea kuzidi.
Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, ameamuru kodi ya dola 45 za kimarekani itozwe kwa kila tani moja ya mafuta ya Urusi kufuatia hatua ya Urusi kufuta ruzuku kwa mafuta inayopeleka nchini Belarus.
Mapipa milioni moja ya mafuta ya petroli ya Urusi hupitia Belarus kila siku ikiwa ni asilimia 20 ya mafuta yanayouzwa nje ya Urusi. Mengi ya mafuta hayo hupelekwa katika viwanda vya kusafishia mafuta nchini Poland na Ujerumani.
Hatua hiyo ya Belarus huenda ikatatiza ugavi wa mafuta kwa muda.